Marko Ji Tianxiang

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wafiadini Wakatoliki wa China.

Marko Ji Tianxiang (Yazhuangtou, 1834 hivi - Yazhuangtou, 7 Julai 1900) alikuwa tabibu wa China aliyefia Ukristo kwa kukatwa kichwa wakati wa Uasi wa Mabondia.

Alinyimwa ekaristi miaka 30 kwa kutokubali kuacha uvutaji afyuni, lakini wakati huo wote aliendelea kusali ili amalize maisha yake kitakatifu, na ndivyo alivyofanya alipokamatwa kwa ajili ya imani yake[1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila mwaka tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 7 Julai[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/61110
  2. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.