Mark Twain

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mark Twain
Mark Twain, Brady-Handy photo portrait, Feb 7, 1871, cropped.jpg
Amezaliwa Samuel Langhorne Clemens
30 Novemba 1835
Missouri, Marekani
Amekufa 21 Aprili 1910
Connecticut, Marekani
Nchi Marekani
Kazi yake Mwandishi
Ndoa Olivia Langdon Clemens
Watoto Langdon, Susy Clemens, Clara Clemens, Jean Clemens

Mark Twain lilikuwa jina la kisanii la Samuel Langhorne Clemens (30 Novemba 1835 - 21 Aprili 1910) aliyekuwa mwandishi nchini Marekani.

Alizaliwa katika mji wa Florida kwenye jimbo la Missouri akaendelea kuwa mwandishi wa magazeti na baadaye nahodha wa meli ya mto Missisippi. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani ilizuia usafiri wa mtoni akaenda magharibi alipojaribu kuchimba dhahabu akaanza tena kuandika kwa gazeti.

Mwaka 1863 alianza kuandika kwa jina la kuchaguliwa "Mark Twain". Jina hili lilitokana na lugha ya mabaharia likimaanisha "alama mbili" kwenye uzi wa kupima kina cha maji chini ya meli ni kina kinachohitajika kwa safari. Kwa jina hili alitoa hadithi za kichekesho zilizopendwa na watu akajenga sifa yake. Akatumwa na magazeti kwa safari akiendelea taarifa za kichekesho juuy a safari zake.

Baadaye alitoa pia riwaya. Kati ya vitabu vyake ambavyo hutazamiwa kama bora ni Huckleberry Finn ambayo ni hadithi ya kijana mzungu anayemsaidia mtumwa wa asili ya Kiafrika kupata uhuru wake katika majimbo ya kusini ya Marekani.

Maandiko[hariri | hariri chanzo]

  • The Adventures of Tom Sawyer (1876)
  • The Prince and the Pauper (1882)
  • Adventures of Huckleberry Finn (1884)
  • A Connecticut Yankee in King Arthur's Court (1889)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]