Nenda kwa yaliyomo

Marino shemasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marino kazini.

Marino shemasi (kisiwa cha Rab, Dalmatia, Kroasya, karne ya 3 - San Marino, 366) alikuwa mchongamawe karibu na Rimini, Italia, aliyejitahidi pia kufikisha wenyeji Wapagani kwenye mwanga wa Injili na uhuru wa Kristo.

Halafu akawa mkaapweke kwenye mlima Titano na shemasi wa Kanisa Katoliki[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na mwanzilishi (301) wa monasteri ambayo ikawa jamhuri ya San Marino, nchi huru yenye jina lake katika rasi ya Italia.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Septemba[2][3]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.