Maria wa Umwilisho Guyart

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Maria alivyochorwa.

Maria wa Umwilisho Guyart (Tours, Ufaransa, 28 Oktoba 1599 - Quebec, Kanada, 30 Aprili 1672) alikuwa mwanamke wa Ufaransa ambaye baada ya kufiwa mume wake alimuacha mtoto wake kwa ndugu akajiunga na monasteri ya Waursula[1][2] akawa mwanzilishi wa monasteri ya aina hiyo katika koloni la New France, ambayo sasa ni sehemu ya Québec, Kanada[3] .

Monasteri nyingine zilifuata na kuchangia uenezi wa Kanisa Katoliki katika eneo hilo la Amerika Kaskazini. Pia Maria alianzisha shule ya kwanza kwa ajili ya wasichana katika bara zima la Amerika[4][5] akitumia pia lugha za Waindio [6].

Alitangazwa rasmi mwenyeheri na Papa Yohane Paulo II tarehe 22 Juni 1980, halafu mtakatifu na Papa Fransisko 3 Aprili 2014[7][8][9].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyofariki dunia[10][11].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Jaenen, Cornelius J., "Marie de l'Incarnation", The Canadian Encyclopedia Archived 25 Septemba 2013 at the Wayback Machine
 2. Joining the monastery required her to leave her young son, and he expressed much difficulty with the separation. Claude tried to storm the monastery with a band of school friends, and could repeatedly be found crying at the gates, trying to enter. She left him in the care of the Buisson family, but the emotional pain of the separation would remain with them both. Later, when her son had become a Benedictine monk, they corresponded candidly about their spiritual and emotional trials.
 3. Sister Mary of Jesus. "Ursulines", L’Encyclopédie de l’histoire du Québec, 1948
 4. Deslandres, Dominique (1987). L'éducation des Amérindiennes d'après la correspondance de Marie Guyart de l'Incarnation. Canada: Sciences Religieuses. 
 5. Deslandres, Dominique (1985). Attitude de Marie de l'Incarnation à l'égard des Amérindiens. Canada: Université McGill. 
 6. Harvey, Tamara (2008). Women and Gender in the Early Modern World : Figuring Modesty in Feminist Discourse Across the Americas, 1633-1700. Aldershot, Hampshire, England: Ashgate, 118. 
 7. "Mary of the Incarnation", Ursulines de l'Union Canadienne
 8. "Saint Marie of the Incarnation Guyart", CatholicSaints.Info, 2010-04-29. (en-US) 
 9. The Anglican Church of Canada celebrates her with a feast day.
 10. Martyrologium Romanum
 11. Ursulines (of the Canadian Union). Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-05-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-28.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

 • Davis, Natalie Zemon. Women on the Margins: Three Seventeenth-Century Lives, Harvard University Press, Cambridge, Massachusetts, 1995.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.