Margerita wa Cortona
Mandhari
Margerita wa Cortona (Laviano 1247 – Cortona 22 Februari 1297) alikuwa mwanamke wa Italia aliyefanya toba katika Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko baada ya kuishi na mwanamume bila ndoa kwa muda wa miaka kumi.
Kwa kushtushwa sana na kifo cha ghafla cha huyo hawara wake, alifidia kwa malipizi makali dhambi za ujanani akazama katika mambo ya mbinguni kwa kujazwa na Mungu karama za pekee sana.
Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Mei 1728.
Sikukuu yake ni tarehe ya kifo chake[1] au 16 Mei.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Catholic encyclopedia: St. Margaret of Cortona
- Eternal Word Television Network, excerpt from "Saints for Sinners" Ilihifadhiwa 1 Machi 2012 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |