Nenda kwa yaliyomo

Mangi Meli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mangi Meli

Picha]] yake halisi.
Amekufa 2 Machi 1900
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanasiasa

Mangi Meli Kiusa bin Rindi Makindara Tarimo (18662 Machi 1900) alikuwa mangi[1] wa Oldmoshi, aliyepambana na Wajerumani kwa kuwashinikiza waondoke katika himaya yake, jambo ambalo Wajerumani walilipinga kwa kudai kuwa baba yake Meli, ambaye alikuwa ameshafariki, ndiye aliyewakaribisha, hivyo hawawezi kuondoka. Jambo lilizua mapambano makubwa na kupelekea kifo chake, ambapo aliuawa kwa kunyongwa na kisha kukatwa kichwa. Chifu wa Marangu, aliyeitwa Mangi Marealle, na chifu wa Machame walikula njama na Wajerumani na kufanikiwa kumkamata Mangi Meli: walinzi wake wote walikubali kuajiriwa katika serikali ya Kijerumani, jambo lililorahisisha kukamatwa kwa Meli, kwani alibaki peke yake bila walinzi, hivyo walipovamia himaya hiyo hawakukumbana na changamoto yoyote. Hii inaonyeshwa udhaifu wa hali ya juu wa serikali ya Kijerumani kwani mtu kama Meli angetakiwa kuachwa na walinzi wake kisha kuanzisha vita ambavyo vingewasambaratisha walinzi wake, hivyo kuleta hali ya ukomavu wa kisiasa, lakini suala la kununua askari wa adui ni udhaifu wa hali ya juu usiofaa kuigwa duniani kote. Tabia ya kusaliti jeshi ni tatizo lililozikumba himaya nyingi za kichifu, hasa kipindi cha utawala wa Kijerumani.

Fuvu lake lilipelekwa Ujerumani, jambo lililosababisha Mangi Meli kuzikwa kiwiliwili pekee. Mpaka leo hii bado taratibu za kufuatilia kurejeshwa kwa fuvu la kichwa chake linaendelea huku mjukuu wake aitwaye Isaria Meli akitumika katika suala hilo la kutafuta fuvu la Meli Ujerumani[2] [3].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Chagga people- history, religion, culture and more". United Republic of Tanzania. 2021. Iliwekwa mnamo 2023-04-08.
  2. "[v Executed Tanzanian hero's grandson takes DNA test to find lost skull]", 20 November 2018. 
  3. Chandler, Caitlin. "Skeletons from Kilimanjaro; East African Families Seek to Reclaim the Remains of Their Ancestors from German Colonial Collections", 23 March 2023. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mangi Meli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.