Mammito Eunice
Eunice Wanjiru Njoki (anaejulikanaa kwa jina la Mammito; alizaliwa Nairobi, 18 Septemba 1993) ni Mkenya anayejihusisha na shughuli za uigizaji, uandishi, utangazaji na uchekeshaji
[[Jamii: Art and feminism 2023]]
Maisha ya awali na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Mammito hakuwahi kupata nafasi ya kumfahamu baba yake mzazi wala hakuwahi kujua hisia azipatazo mtu anapokua na baba.[1] Mama yake, Nancy Njoki, alimlea na kumkuza peke yake.[2] Alikulia katika makazi duni ya Kibera.[3]. Alipata elimu yake ya msingi kutoka shule ya Laini Saba. Kupata mlo mmoja pekee ndani ya Kibera ililazimu kupambana.[4] Kwasababu Maisha katika makazi haya yalikua na changamoto nyingi, mama yake alikuwa mkali sana na hakumruhusu acheze na watoto wa majirani.[1]
Mammito alijiunga na darasa la kwanza katika shule ya msingi Laini Saba mwaka 2001. Alifanya mitihani yake ya KCPE mwaka 2007. Baada ya apo, alijiunga na shule ya sekondari ‘’Gatero Girls High School, Nyahururu’’[3] mwaka 2008 ambapo alisoma mpaka kidato cha tatu. Mwaka 2011 alibadili shule na kujiunga na Silanga Mixed Secondary School, Kibera ambapo huko alifanya mitihani ya KCSE mwaka 2011. Alisoma Elimu ya maendeleo ya jamii kutoka chuo kikuu cha Mount Kenya.[onesha uthibitisho]
Kwa kipindi hicho, alijihusisha sana na uchekeshaji, uchezaji muziki na mashairi, vyote hivi mama yake na shangazi walivipinga kwa nguvu kwa madai ya kuwa vinamfanya awe kituko.[3] Kutokana na hilo, alikua mkaidi na mbishi, kitendo kilichosababisha ahamishiwe kijijini Murang'a akaishi na bibi yake. Akiwa Murang'a, alikua akimsaidi bibi yake kuuza nguo za shule na nguo za aina nyingine.
Baada ya hapo, mnamo mwaka 2015 Mammito alijiunga na chuo kikuu cha Mount Kenya (Mount Kenya University), alisoma na kupata astashahada ya maendeleo ya jamii. Akiwa chuo, alijiunga na kikundi cha uigizaji. Katika mojawapo ya maonyesho ya vipaji, ‘’ Nilisajili kama muimbaji, lakini nilipofika jukwaani, nikaaza kutoa vichekesho. Majaji walifurahia sana na walinipigia makofi kwa kusimama. Ni kwa wakati huo ndipo nilipogundua nina uwezo wa kuwa mchekeshaji."[5]Alimaliza elimu yakw mwaka 2016.
Alipata jina la Mammito, kutoka kwa marafiki zake ambao walikua wanaitana Mammito.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]2015 mpaka sasa
[hariri | hariri chanzo]Baada ya chuo, Mammito alianza kutafuta kazi kama mtumishi wa uma, lakini hakufanikiwa kupata. Hakuwahi kufikiria kufanya uchekeshaji kama kazi yake. Lakini alipokosa kazi kabisa, aliomba nafasi kutoeza katika vipindi vya Churchill Show.[3]. Kwa mara kadhaa, alishindwa kushawishi[5] na alitolewa na kurudishwa kwa kukosa kujiamini na umiliki wa jukwaa, baadaye aliitwa tena kwani utani wake ulikuwa unachekesha sana. Hali hii iliendelea kwa muda mpaka alipopata nafasi.[3] mwaka 2015.
Mwaka 2015 wakati wa maonyesho yake ya kwanza ndani ya Churchill Show, alikua na uoga mwingi sana,[5] kiasi kwamba hakuna aliyecheka. "Ni kama vile nilikua natoa hotuba, hakukua na kitu zaidi ya mwangwi. Kuna mud ahata nilisahau mistari yangu, nikabaki kutazama hadhira na kuondoka jukwaani, nilidhalilika sana, nikabaki kulia tu."
Mwaka 2017, Mammito alikua kwenye ratiba ya kufanya maonyesho katika tamasha la Kigali International Comedy Festival lililofanyika Novemba.[6]
Mwaka 2018 Mammito alishiriki katika onyesho la Anthony Bourdain maelezo ya Maisha yake.[7] Mnamo Juni 2018, alitumbuiza katika Seka Festival Season 4 huko Kigali. Rwanda.[8][9] Hiyo hiyo Juni 2018, alifanya maonyesho katika tamasha la East Africa Comedy Show lililofanyika Kenyatta International Convention Centre (KICC).[10] Disemba 2018, alirudi tena Rwanda kufanya maonyesho wakati wa Evening of Laugh Comedy Show[9]
Mnamo January 2019, Mammito aliongoza katika Saturday Night Comedy kwenye mgahawa wa ‘’Blues Restaurant’’ jijini Nairobi.[11] Mammito alitumbuiza katika maonyesho ya 2019 Laugh Festival yaliyofanyika KICC.[12][13] Agosti 2, alishiriki katika maonyesho ya Queens of Comedy nchini Botswana.[14][15][16]
Maisha yake
[hariri | hariri chanzo]Mammito ana ndugu wawili.[3] Mwaka 2018, alipiga picha akiwa na Edwin Butita, hii ilisababisha uvumi kwamba ana mimba.[17][18] Kukanusha uvumi huo, alisema kwamba walipiga picha hiyo baada ya kutoka kupata mlo wa mchana.
Mammito ni Mkristo.
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Televisheni
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Tukio | Uhusika | Maelezo | Mtandao |
---|---|---|---|---|
2017 – hadi sasa | Churchill Show | Mwenyewe | NTV Kenya | |
2018 | Anthony Bourdain: Sehemu hazitambuliki | Mwenyewe | Sehemu ya 12: kipande cha 1 |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 Okoth, Brian (27 Januari 2016). "#WCW: Confessions of comedienne Mammito; difficulty in relating with men is one". edaily. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-26. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Mammito |Kenyan Comedian- Biography, Age, Real names, Family, Photos". Life Issues in Kenya. 4 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 Kamau, Richard (11 Aprili 2016). "Everything You Need to Know About Churchill Show Comedienne Mammito". Nairobi Wire. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link) - ↑ Maina, Njange (31 Oktoba 2019). "Kibra's hall of fame: 10 stars who've made it in life". K24 TV. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link) - ↑ 5.0 5.1 5.2 "EUNICE "MAMMITO" NJOKI Carving her niche in stand-up comedy". Parents Magazine Africa. 3 Februari 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-26. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Batamuriza, Natasha (1 Novemba 2017). "Renowned Comedians To Grace The Kigali International Comedy Festival". Taarifa Rwanda. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-10. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2019.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Anthony Bourdain: Parts Unknown" Kenya (TV Episode 2018), IMDb, iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2019
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Akayezu, Jean De Dieu (10 Machi 2018). "Ibyamamare bya Afurika mu rwenya bizahurira I Kigali mu iserukiramuco rimaze umwaka ritegurwa" [Comedians from Africa to Meet in Kigali for a Festive that Has Been in Preparations for One Year]. Ukwezi (kwa Kinyarwanda). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-10. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2019.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 9.0 9.1 Opobo, Moses (13 Desemba 2018). "Comedy Knights in 'Evening of Laugh' comedy show". The New Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Desemba 2018. Iliwekwa mnamo 4 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Musungu, Nahashon (10 Juni 2018). "Kansiime loses her luggage but steals the show on comedy night". Nairobi News. Iliwekwa mnamo 3 Novemba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link) - ↑ Oneya, Faith (16 Januari 2019). "Kenya: Stand-Up Comedy Where No Topic Is Off Limits". Daily Nation. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link) - ↑ Nkurunzinza, James Peter (25 Julai 2019). "Rwandan comedian to perform at the 'Laugh Festival' in Nairobi". The New Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kagonye, Fredrick (29 Julai 2019). "'Wamlambez' dominates Laugh Festival". The Standard. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link) - ↑ Nokuthula (30 Julai 2019). "Queens Of Comedy Have The Best Medicine". TSWAlebs. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-04. Iliwekwa mnamo 3 Novemba 2019.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Major Moves Comedy Lines Up All Female Comics". Mining & Travel. 25 Julai 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-10. Iliwekwa mnamo 3 Novemba 2019.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Motimane, Ame (5 Agosti 2019). "The Monitor :: Queens Of Comedy Warm Up Masa Audience". The Monitor. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-09-05. Iliwekwa mnamo 3 Novemba 2019.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Monicah, Shanniq (24 Januari 2018). "Is Churchill's female comedian Mammito pregnant for Butita? - Evewoman". standardmedia.co.ke. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link) - ↑ Kerongo, Grace (3 Oktoba 2018). "Usitukane Wakunga! Pregnant Mammito causes panic when she goes into false labour (Video)". Classic 105. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-10. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mammito Eunice kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |