Mamadou Sidiki Diabate
Mamadou Sidiki Diabaté (alizaliwa Septemba 23, 1982) ni mpigaji maarufu wa kora na mjeli mwenye asili ya Wamandé[1] kutoka mjini Bamako, Mali. Mamadou ni kizazi cha 71 cha wachezaji wa kora katika familia yake na ni mtoto wa Sidiki Diabaté.
Mamadou Sidiki Diabaté, anayejulikana zaidi kwa kifupi kama "Madou," alizaliwa mnamo tarehe 23 Septemba, 1982, huko mjini Bamako, Mali. Mamadou ni Muislamu na ni mtoto wa mwisho wa Sidiki Diabaté na Mariam Kouyaté. Familia yake ina urithi mrefu katika utamaduni wa masimulizi ya mdomo ya wajalis (wakati mwingine huitwa djeli), au wagrioti. "Jali" ni neno la Kimandinka lenye maana ya msanii au msimuliaji wa hadithi anayehifadhi utamaduni wa masimulizi ya kale ya Wamande. Akipitisha historia hiyo na utamaduni kutoka kizazi kimoja hadi kingine, kutoka kwa baba hadi mtoto.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mandé," mara nyingi hutumika kuelezea Madou na familia yake, ni jina la kitamaduni linalojumuisha makabila kadhaa katika Afrika Magharibi, ikiwa ni pamoja na (ingawa si pekee) Mandinka, Maninka (au "Malinke"), Sarakole, Bambara, na Dyula, ambao wanakaa hasa Gambia, Senegal, Guinea, Mali, maeneo ya kaskazini ya Ivory Coast, na maeneo ya magharibi ya Burkina Faso. Tazama: R. Skinner, Artistiya 2009. p. 212"
- ↑ "Back Matter". Mande Studies. 19. 2017. doi:10.2979/mandestudies.19.2017.bm.
Makala hii ni sehemu ya warsha ya kuhariri Wikipedia huko MUM. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari. |