Majadiliano ya mtumiaji:Moseskehengu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo - hata kuitafsiri kutoka katika Wikipedia kwa lugha nyingine. Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wa sanduku la mchanga. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike pekee kwenye ukurasa wako wa mtumiaji baada ya kufungua akaunti. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho. Ujue miiko: usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje wala matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo). Karibu sana!

Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non speaker better first communicate with one of our admins who will advise you. You find them at Wikipedia:Wakabidhi. And btw: NEVER post computer translated texts (like google-translate, mediawiki Content Translation etc.) nor copied texts/images from other webs to this site! And do not use links to commercial pages.

--Mr Accountable (majadiliano) 18:21, 9 Desemba 2009 (UTC)

Neptune[hariri chanzo]

Salam, Moses. Kaka, nimeweka kitangazo cha kuonyesha makala zipo mbili, lakini kila nikiweka wewe unatoa. Kigezo kile kinaonyesha kwamba makala zipo mbili. Hivyo ni kiasi cha kufuata kurasa iliyoelekezwa - angalau ungeelewa somo. Hii si nzuri. Ulichotakiwa kufanya ni kujadili na si kufuta au kuondoa kile kigezo. Japokuwa makala yako inaonekana kuwa kubwa zaidi ya ile ya awali. Basi salam ndiyo hizo - kila la kheri.--MwanaharakatiLonga 06:22, 7 Januari 2010 (UTC)

Utawala wa Kijiji[hariri chanzo]

Bwana Moses, nimeona sasa tu makala Utawala wa Kijiji - Tanzania uliyoanzisha. NApenda kukushukuru na kukupongeza. Je unaweza kuendelea na vichwa hivi? Nisipokosei sasa hivi una mengine ukiwa ndani ya mitihani ya kumaliza masomo yako. Nakutakia heri na baraka nitafurahia kusikia kutoka kwako. --Kipala (majadiliano) 16:23, 27 Aprili 2010 (UTC)