Majadiliano ya mtumiaji:Felix sakalani
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
Idd ninga (majadiliano) 09:17, 19 Juni 2021 (UTC)
Tafadhali usahihishe
[hariri chanzo]Felix naona umejitahidi kutunga makala kadhaa. Nikipitilia naona umetumia mara kadhaa marejeo (vyanzo) ambayo hayana uhusiano kabisa na mada ya mchango wako. Mifano michache:
- Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu ya Afrika Kusini - marejeo ni "Wartime Basketball: The Emergence of a National Sport during World War II"
- Binti (filamu ya 2021) umeweka chanzo kuhusu "Women in Pre-colonial Africa: East Africa"
- Besieged (filamu) uliweka vyanzo kuhusu "Kesi katika LAs Vegas, Marekani" na " "All-weather ultraviolet solar spectra"
- Malkia wa Afrika (filamu) uliweka tena marejeo ya ajabu sana yasiyolingana; pia umetafsiri jina la filamu ambayo ni kosa, maana majina halisi ya kigeni hayatafsiriwi kama huna ushahidi wa tafsiri iliyotokea tayari (filamu hii haikutafsiriwa kwa Kiswahili). Kwa njia hiyo uliunda makala ingawa makala The African Queen iko tayari.
Ninaomba uniandikie na kueleza kwa nini ulichagua marejeo hayo. (ama hapa au kwenye ukurasa wangu wa majadiliano au kupitia "Email this user" kwenye menyu ya ukurasa wangu) Kipala (majadiliano) 19:40, 2 Septemba 2022 (UTC)
- boss mimi sijatunga marejeo tatizo ni kwamba may zbe zile makala za mwanzo zilikuwa kwa english tulikuwa tunazifanyia transilation dno zilikuwa na shida ya references because i didn't change any thing kwanye swala zima la references nimefanya kama nilivo fundishwa nadhani hapa itabidi kupitia references before hauja insert kwa translated article, references zilizopo ndo zile zile nilizo zitoa kwa makala husika boss wangu Felix sakalani (majadiliano) 18:48, 18 Septemba 2022 (UTC)