The African Queen
The African Queen (Filamu) ni filamu ya matukio iliyotoka mwaka 1951 kutoka Uingereza na Marekani iliyochukuliwa kutoka kwenye riwaya ya mwaka 1935 yenye jina sawa ya C. S. Forester.[1][2]Filamu hii iliongozwa na John Huston, Sam Spiegel na John Woolf wakiwa watayarishaji[3].Mswada wa filamu hii ulirekebishwa na James Agee, John Huston, John Collier, na Peter Viertel. Picha zake zilipigwa kwa teknolojia ya Technicolor na Jack Cardiff, na muziki wake ukapangwa na Allan Gray. Filamu hii imewashirikisha waigizaji Humphrey Bogart (ambaye alishinda Tuzo ya Akademi ya Mwigizaji Bora wa Kiume, ikiwa ndiyo Oscar yake pekee) na Katharine Hepburn, pamoja na Robert Morley, Peter Bull, Walter Gotell, Richard Marner, na Theodore Bikel. The African Queen ilichaguliwa kuhifadhiwa kwenye Daftari la Kitaifa la Filamu la Marekani mwaka 1994, huku Maktaba ya Congress ikiitambua kama filamu yenye "umuhimu wa kitamaduni, kihistoria, au kisanaa."
Wahusika
[hariri | hariri chanzo]- Humphrey Bogart ambaye alicheza kama Charlie Allnut
- Katharine Hepburn ambaye alicheza kama Rose Sayer
- Robert Morley[4] ambaye alicheza kama Reverend Samuel Sayer, "The Brother"
- Peter Bull[5] ambaye alicheza kama kapteni wa Königin Luise
- Theodore Bikel ambaye alicheza kama afisa wa kwanza wa Königin Luise
- Walter Gotell ambaye alicheza kama afisa wa pili wa Königin Luise
- Peter Swanwick ambaye alicheza kama afisa wa kwanza wa Fort Shona
- Richard Marner ambaye alicheza kama afisa wa pili wa Fort Shona
- Gerald Onn ambaye alicheza kama afisa mdogo wa Königin Luise (uncredited)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The African Queen (1951) at Reel Classics". www.reelclassics.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-01-06. Iliwekwa mnamo 2022-08-10.
- ↑ "The African Queen", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2026-07-23, iliwekwa mnamo 2026-07-25
- ↑ "The African Queen", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2026-07-23, iliwekwa mnamo 2026-07-25
- ↑ "Robert Morley", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2026-07-18, iliwekwa mnamo 2026-07-25
- ↑ "Peter Bull", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2026-07-05, iliwekwa mnamo 2026-07-25