Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu ya Afrika Kusini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (BNL) ni ligi ya mpira wa kikapu ya kiume ya nchini Afrika Kusini. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 ligi imekuwa ikichezwa na timu za klabu za kiume pekee [1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ilianzishwa mwaka 1993 kama Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu, ilivunjwa mwaka 1996. Ligi hiyo ilibadilishwa jina na kuitwa Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu mwaka 2013. Msimu wa BNL wa 2018 ulianza Agosti, wa 3 na kumalizika Oktoba, 27. Kwa mara ya kwanza kabisa, michuano hiyo ilitwaliwa na Soweto Panthers [2]

Mnamo 2016 ligi hiyo ilifanya majaribio ya kitengo cha wanawake huko Gauteng, The Sturdy Stars ilishinda taji hilo mwaka huo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "APPENDIX A.", Wartime Basketball (UNP - Nebraska): 311–313, iliwekwa mnamo 2022-09-02 
  2. "APPENDIX A.", Wartime Basketball (UNP - Nebraska): 311–313, iliwekwa mnamo 2022-09-02