Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Brayson Mushi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Idd ninga (majadiliano) 10:07, 2 Machi 2022 (UTC)[jibu]

Kuondoa Kigezo

[hariri chanzo]

Salamu Brayson, iwapo utakuta kigezo chochote kama TAFSIRI YA KOMPYUTA, tafadhali usikitoe kama makala hiyo haijfanyiwa marekebisho, Amani sana Idd ninga (majadiliano) 22:01, 23 Aprili 2022 (UTC)[jibu]

Vyanzo vya Kiingereza

[hariri chanzo]

Tazama katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Leonard_Dembo ulikuwa umeweka vyanzo vinavyotokana na Wikipedia ua Kiingereza, kumbuka kwamba makala kutoka katika Wikipedia ya Kiingereza haiwezi kutumika kama Chanzo katika Wikipedia ya Kiswahili,Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 23:10, 6 Mei 2022 (UTC)[jibu]

GMA awards

[hariri chanzo]

Salamu Brayson, naona umeanzisha mfululizo ya vimakala kama 19th GMA Dove Awards. Je hizo makala zina faida gani? Kwa bahati mbaya ni bute usiponanzisha kwanza makala inayoeleza "GMA Dove Award" ni kitu gani, halafu kuilink ndani ya vimakala. Jinsi zilivyo naona hazieleweki kabisa. Kipala (majadiliano) 06:33, 13 Mei 2022 (UTC)[jibu]

Salamu Brayson,Nishauri kwenye makala zawachezaji unazoanzisha sasa badala ya kuweka kigezo (mbegu-mtu) uweke mfano(Mbegu-cheza-mpira),AMANI SANA. Justine Msechu (majadiliano)

Tazama katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Rolf_Harris na baadhi ya makala nyingine ulizoanzisha, zina lugha ambayo haieleweki na haipo katika mpangilio mzuri,ni bora kuhakikisha lugha unayotumia ni lugha iliyo sawa na inayoeleweka, chukulia mfano umandika Mara nyingi alitumia vyombo visivyo vya kawaida katika maonyesho yake alicheza didgeridoo na stylophone na anajulikana kwa uvumbuzi wa bodi ya wobble.Harris alihukumiwa mwaka wa 2014 wa unyanyasaji wa kijinsia wa wasichana wanne wa chini, ambayo ilimaliza kazi yake kwa ufanisi, aina ya maneno kama hayo hayapo sawa, unaweza rekebisha makala zako ulizoanzisha kabla ya kuendelea kuleta makala nyingine, ili kupunguza mzigo wa kuwepo kwa makala nyingi zisizo na ubora, Amani sana Idd ninga (majadiliano) 06:09, 6 Aprili 2023 (UTC)[jibu]

Angalia pia katika makala hii ya Burl Ives kuna dalili kuwa umetumia tafsiri ya mshine, tazama pia katika makala ya Mary Chapin Carpenter na makala ya Roy Acuff, makala nyingi ulizoanzisha bado hazipo sawa, pitia kwanza makala nyingi na ujifunze zaidi namna nzuri na bora ya kuanzisha makala,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 06:17, 6 Aprili 2023 (UTC)[jibu]
Habari, ndio nimeona makosa yangu naomba niyarekebishe. Brayson Mushi (majadiliano) 12:55, 6 Aprili 2023 (UTC)[jibu]
Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.