Mafuta ya wagonjwa
Mandhari
Mafuta ya wagonjwa (kwa Kilatini: Oleum Infirmorum) ni mafuta yaliyobarikiwa yanayotumiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali (Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Wakatoliki wa Kale, baadhi ya Waanglikana n.k.) katika sakramenti ya Mpako wa wagonjwa.
Kanisa la Kilatini
[hariri | hariri chanzo]Katika Kanisa la Kilatini mafuta ya zeituni au mimea mingine yanabarikiwa na askofu mbele ya mapadri na waumini wengine wa jimbo lake, kwa kawaida asubuhi ya Alhamisi kuu.
Kama padri anapaswa kumpa sakramenti hiyo mgonjwa lakini hana mafuta hayo, anaweza kubariki mwenyewe mafuta ambayo atampaka mgonjwa huyo kwa kawaida katika paji la uso na mikononi.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mafuta ya wagonjwa kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |