Mafuta ya wakatekumeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aina ya tabenakulo ya mafuta matakatifu vinapotunzwa kwa heshima krisma, mafuta ya wagonjwa na mafuta ya wakatekumeni.

Mafuta ya wakatekumeni (kwa Kilatini: Oleum Catechumenorum) ni mafuta yaliyobarikiwa yanayotumiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali (kama Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Wakatoliki wa Kale n.k.) kabla ya kumpa mtu sakramenti ya ubatizo ili kumuimarisha katika mapambano ya kiroho yanayodaiwa na maisha ya Kikristo.

Kanisa la Kilatini[hariri | hariri chanzo]

Katika Kanisa la Kilatini mafuta hayo yanabarikiwa na askofu mbele ya mapadri na waumini wengine wa jimbo lake, kwa kawaida asubuhi ya Alhamisi kuu.

Kanisa la Kiorthodoksi[hariri | hariri chanzo]

Huko padri anabariki mwenyewe mafuta baada ya kubariki maji ya ubatizo.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mafuta ya wakatekumeni kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.