Dalmatia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.2+) (Roboti: Imeongeza be:Далмацыя
d r2.6.5) (Roboti: Imeongeza az:Dalmaçiya
Mstari 21: Mstari 21:
[[an:Dalmacia]]
[[an:Dalmacia]]
[[ar:دالماسيا]]
[[ar:دالماسيا]]
[[az:Dalmaçiya]]
[[be:Далмацыя]]
[[be:Далмацыя]]
[[be-x-old:Далмацыя]]
[[be-x-old:Далмацыя]]

Pitio la 23:48, 3 Machi 2013

Dalmatia (buluu-nyeusi) katika Kroatia - (buluu yote)

Dalmatia (Kikroatia: Dalmacija, Kiitalia Dalmazia) ni jina kwa nchi ya pwani la Adria katika kusini la Kroatia.

Inaanza kwenye kisiwa cha Rab upande wa kaskazini na kuendelea hadi mpaka wa Montenegro upande wa kusini. Upande wa bara mwisho wake ni mpaka wa Bosnia na Herzegovina.

Wakazi wengi huishi pwani lakini sehemu za bara kuna watu wachache. Uchumi unategemea hasa utalii na watalii kutoka pande nyingi za Ulaya wanakuja hapa kwa burudani kando la bahari katika miezi pasipo na baridi. Kati ya watalii milioni 10 - 11 wanaofika Kroatia kila mwaka idadi kubwa kabisa inalenga pwani la Dalmatia. [1]

Kihistoria hii ilikuwa eneo la miji-dola kwenye pwani iliyostawi kutokana na biashara ya baharini. Kati ya miji hii ni Split, Zadar, Šibenik na Dubrovnik. Kwa karne 3 kati ya mwaka 1400 hadi 1797 pwani la Dalmatia ilikuwa chini ya utawala wa jamhuri ya Venezia. Hii inaeleza hali ya kwamba miji mingi ya pwani inafanana na miji ya Italia kutokana na namna ya ujenzi ya nyumba na makanisa na mpangilio wa miji. Tangu 1797 hadi 1918 Dalmatia ilikuwa jimbo la ufalme wa Austria, baadaye Austria-Hungaria. Baada ya 1918 imekuwa sehemu ya Kroatia ndani ya Yugoslavia hadi kuporomoka kwa Yugoslavia mwaka 1991.

Jina la "Dalmatia" limetokana na zamani za Roma ya Kale na hasa kabila la "Dalmatae" waliopigana na Waroma wa Kale. Leo hii wakazi walio wengi ni Wakroatia.

Marejeo

  1. Takwimu kuhusu idadi ya watalii katika Kroatia http://reports.aiidatapro.com/CBE/Tourism_2009.pdf

Kigezo:Link FA