Mirihi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: gv:Mart (planaid)
d roboti Nyongeza: gan:火星
Mstari 82: Mstari 82:
[[frp:Mârs (planèta)]]
[[frp:Mârs (planèta)]]
[[ga:Mars (pláinéad)]]
[[ga:Mars (pláinéad)]]
[[gan:火星]]
[[gl:Marte (planeta)]]
[[gl:Marte (planeta)]]
[[gu:મંગળ (ગ્રહ)]]
[[gu:મંગળ (ગ્રહ)]]

Pitio la 12:38, 8 Juni 2008

Mirihi (Mars)

Mirihi (pia: Meriki, Mars) (kutoka Kiarabu المريخ al-miriikh) ni sayari ya nne katika mfumo wa jua na sayari zake. Hivyo ni sayari jirani ya dunia yetu. Kutokana na rangi yake imeitwa "sayari nyekundu". Ina miezi miwili midogo inayoitwa Phobos na Deimos.

Sura ya Mirihi inafanana zaidi na dunia yetu kati ya sayari zote ilhali haina joto au baridi kali mno.

Mzingo wake wa kuzunguka jua

Mirihi inazunguka jua kwa umbali wa kilomita milioni 206.62 hadi 249,23 ikitumia karibu miaka miwili ya kidunia (mwaka 1 siku 321 na masaa 18) kwa mzingo wake. Mzingo wa kuzunguka jua imenama 1.85° kutoka ekliptiki.

Tabia za kifisikia

Ulinganisho wa ukubwa: Picha zenye skeli ileile za Dunia na Mirihi kandokando

Kipenyo cha Mirihi ni 6.794 km (takriban nusu kipenyo cha dunia); eneo la sura yake ni nusu ya eneo la sura ya dunia; masi yake ni sehemu ya kumi tu ya masi ya dunia.

Mirihi inazunguka kwenye kipenyo chake katika masaa 24 na dakika 37 za kidunia. Kipenyo cha mzunguko kimenama 25° 12' dhidi ya njia ya mzingo wa kuzunguka jua. Hali hii inasababisha majira ya joto na ya baridi inayofanana na dunia lakini kutokana na muda wa mwaka hata muda ya majira ni ndefu kuliko duniani.

Angahewa

Angahewa ya Mirihi ni haba sana yenye shindikizo la pascal 750 tu yaani 0.75% ya shindikizo la hewa duniani. Hewa yake ni hasa dioksidi ya kaboni (95%), nitrogeni (3%), argoni (1.6%) ikionyesha pia dalili hafifu za oksijeni na maji.

Kutokana na uhaba wa hewa joto lililopokelewa kutoka kwa jua lapotea haraka sana hivyo kuna baridi wakati wa usiku. Halijoto karibu na ikweta wakati wa majira ya joto ni kati ya 20°C wakati wa mchana na hadi –85°C wakati wa usiku.

Mirihi ina upepo na mawingu. Nchani pana barafu ya daioksidi ya kaboni pia barafu ya maji inayoyeyuka wakati wa joto na kusababisha mawingu. Majira kati ya baridi na joto hutokea dhoruba kali zinazotupa vumbi nyingi hewani ya kufunika sehemu kubwa za uso wa sayari.

Uso wa Mirihi

Eneo lilipotelemka chombo cha angani cha NASA Vikinglander

Uso wa sayari inaonyesha tofauti kubwa kati ya kizio cha kaskazini na kizio cha kusini. Kaskazini pana hasa tambarare, kusini kuna hasa milima na nyanda za juu. Kutokana na uhaba wa maji hakuna bahari au mito lakini kuna dalili kama mabonde makavu yanayoonyesha ya kwamba zamani mito ilikuwepo.

Tambarare za kaskazini zina mchanga na vumbi nyingi. Maeneo haya yana rangi tofauti mengine yanaonekana meusimeusi kwa darubini. Maeneo haya yaliaminiwa zamani ndiyo bahari hivyo yaliitwa kwa jina "mare" (Kilatini: bahari) kama vile Mare Erythraeum au Mare Sirenum.

Katika kizio cha kusini ndipo milima mikubwa inayojulikana ulimwenguni hadi leo. Mlima mkubwa kabisa ndio Olympus Mons (Mlima wa Olimpiki) ukiwa na urefu kwenda juu wa 26 km. Mazingira yake yenye milima mikubwa mengine huitwa Tharsis pana pia volkeno.

Ncha za kaskazini na kusini zina vilele vya barafu. Sehemu kubwa ya barafu hii ni daioksaidi ya kaboni iliyoganda, sehemu ndogo ni barafu ya maji. Kilele cha barafu cha kaskazini kina kipenyo cha 1000 km wakati wa majira ya joto; unene wa barafu hukadiriwa kuwa 5 km. Kilele cha barafu cha kusini ni ndogo kipenyo chake ni 350 km tu, unene wake takriban 1.5 km.

Katika eneo la ikweta ya Mirihi kuna bonde la ufa kubwa sana lenye urefu wa 4000 km lina kina hadi 7000 m.

Vyombo vya angani vimefika Mirihi na kutuma picha. Hali halisi uso wa sayari ni jangwa kubwa sana.

Dhoruba ya vumbi Mirihini (picha zilipigwa na chombo cha NASA 2004)

Mifereji

Mirihi ni sayari iliyoaminika kuwa na uhai hata aina ya wanadamu. Tofauti na sayari jirani nyingine ya dunia yetu ambayo ni Zuhura (au Ng'andu) uso wa Mirihi unaonekana kwa darubini. Katika karne ya 19. BK wanaastronomia hasa Mwitalia Giovanni Schiaparelli waliona alama kama mistari kwenye uso wa Mirihi. Schiaparelli aliita mistari hii kwa neno la Kiitalia "canali" yaani mifereji. Jina hili lilisababisha watu wengi kujiuliza je mifereji imepatikana namna gani? Halafu katika eneo la mistari hii mabadiliko ya rangi ilionekana. Haya yote yamesababisha tuhuma na makadirio ya kuwa mifereji imechimbwa kwa kusidi la kupeleka maji maeneo makavu yanayomwagiliwa na kuonyesha rangi ya mazao kimajira. Kumbe lazima kuna wachimbaji kwa hiyo wako aina ya watu wenye utamaduni. Watu hawa waliozaliwa katika fikra za wanaastronomia na waandishi wa vitabu walijulikana kote duniani baadaye imani ilianza ya kuwa wanatutembelea duniani.

Leo imegunduliwa ya kwamba sehemu kubwa ya mistari iliyoripotiwa na Schiaparelli haiko tena si mifereji. Sababu ya kuziona ilikuwa hali ya darubini ya zamani pamoja na kuchoka kwa macho ya watazamaji. Mistari kadhaa iko kweli lakini si mifereji iliyochimbwa bali mabaki ya mito ya kale kutoka zamani Mirihi ilipokuwa bado na maji. Mabadiliko katika rangi kwenye sehemu ya uso za Mirihi yamejulikana ni kutokana na dhoruba kubwa yanayorusha vumbi kwenye angahewa.