Nitrojeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nitrogeni)


Nitrojeni (Nitrogenium)
Nitrojeni ndani ya chombo katika hali ya kiowevu ikiwa na halijoto chini ya -182.95 °C
Nitrojeni ndani ya chombo katika hali ya kiowevu ikiwa na halijoto chini ya -182.95 °C
Jina la Elementi Nitrojeni (Nitrogenium)
Alama N
Namba atomia 7
Mfululizo safu Simetali
Uzani atomia 14.0067
Valensi 2, 5
Densiti 1.251 g/L
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 63.15 K (−210.00 °C)
Kiwango cha kuchemka 77.36 K (−195.79 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0,03 %
Hali maada gesi

Nitrojeni ni elementi yenye namba atomia 7 katika mfumo radidia na uzani atomia 14.0067. Alama yake ni N. Ina elektroni 5 katika ganda la nje.

Duniani haipatikani kama atomi za pekee lakini kama molekuli ya N2 inayounganisha atomi mbili za N. Katika hali hii ni gesi isiyo na ladha au harufu. Gesi hii ni sehemu kubwa ya hewa tunayopumua ambamo kuna asilimia 78 za nitrojeni na 21 % za oksijeni.

Nitrojeni imo ndani ya kila kiumbehai hakuna uhai duniani bila N. Shambani huongezwa kama mbolea kwa kukuza mimea.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nitrojeni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.