Luteti
Mandhari
(Elekezwa kutoka Lutetium)
Luteti safi kwa maumbo tofauti
| |
Jina la Elementi | |
Alama | Nd |
Namba atomia | 71 |
Mfululizo safu | Lanthanidi |
Uzani atomia | 174.9668 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 9, 2 |
Densiti | 9.841 g/cm3 (hali mango) |
Kiwango cha kuyeyuka | °K 1225 |
Kiwango cha kuchemka | °K 3675 |
Asilimia za ganda la dunia | 0.7 ppm |
Hali maada | mango |
Luteti (lutetium) ni elementi ya kimetali yenye alama Lu na namba atomia 71. Rangi yake ni nyeupe-kifedha.
Katika orodha ya elementi imepangwa katika kundi la metali za mpito na kati ya lanthanidi. Tabia zake hulingana na lanthanidi kwa jumla.
Iligunduliwa mwaka 1907 na wanakemia mbalimbali; ilhali Mfaransa Georges Urbain alikuwa wa kwanza kutoa taarifa zake alipewa haki ya kuchagua jina akateua Luteti kufuatana na Lutetia, jina la kale la Paris.
Ilhali ni metali haba ambayo ni vigumu kuisafisha, tena kwa gharama kubwa, hakuna matumizi mengi ya kibiashara. Inatumika kama kichocheo katika uharibikaji kijoto wa mafuta asilia na michakato mingine ya kikemia.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Luteti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |