Louis Pasteur

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Louis Pasteur
Pasteur katika maabara

Louis Pasteur (27 Desemba 182228 Septemba 1895) alikuwa mwanasayansi kutoka nchini Ufaransa. Aliweka misingi ya mikrobiolojia yaani utaalamu wa viumbe vidogo sana ambavyo huonekana kwa hadubini tu.

Pamoja na mke wake alifanya utafiti ulionyesha ya kwamba magonjwa mara nyingi yanasababishwa na vidubini kama bakteria. Aliendelea kugundua njia za kuongeza kinga cha mwili dhidi ya magonjwa kwa njia ya chanjo akagundua chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa na kimeta.

Aligundua pia mbinu wa kutunza vyakula kama maziwa kwa muda mrefu na mbinu huu huitwa upasteurishaji kwa heshima yake. Kuharibika kwa vyakula kunazuliwa kwa kupasha vyakula joto kiasi cha 70 °C na kuvifunga katika chombo bila hewa kuingia.

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: