Nenda kwa yaliyomo

Kimeta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Majibu ya ngozi baada ya mtu kupatwa na kimeta
Majibu ya ngozi baada ya mtu kupatwa na kimeta

Kimeta (kwa Kiingereza: Anthrax) ni ugonjwa wa kuambukiza. Wanadamu wote na wanyama wanaweza kupata huu ugonjwa.

Inasababishwa na bakteria bacthus anthracis. Pia huwapata wanyama wenye kwato kama vile ngamia na twiga.

Spora au chembe za bakteria zinaweza kuishi kwa mamia ya miaka. Kwa kawaida watu hupata ugonjwa huo kutoka kwa wanyama. Kwa kawaida haiambukizi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Kimeta kinaweza kutibiwa na antibiotiki. Pia kuna chanjo dhidi yake. Ikiwa haitatibiwa mapema, ugonjwa wa kimeta husababisha kifo.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimeta kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.