Leokadi na Lusori
Mandhari
Leokadi na Lussori (kwa Kifaransa: Léocade na Ludre; walizaliwa karne ya 3 - walifariki Déols, leo nchini Ufaransa) walikuwa baba na mtoto wake walioishi Ufaransa ambapo Leokadi, seneta wa Dola la Roma, alipelekwa kama mtawala akapokea wamisionari wa kwanza huko Bourges akaongokea Ukristo akageuza nyumba yake kuwa kanisa akajitahidi kuinjilisha pia.
Lussori aliwahi kufariki dunia, akiwa amevaa nguo nyeupe za ibada.[1].
Gregori wa Tours aliandika habari zao [2].
Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki wa Waorthodoksi kama watakatifu.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Novemba[3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/77835
- ↑ De gloria confessorum, XCII
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |