Nenda kwa yaliyomo

Landelini wa Crespin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Landelini akimuomba Bikira Maria.

Landelini wa Crespin (pia: wa Lobbes; Pas-de-Calais, 625 hivi - Crespin, Hainault, leo nchini Ufaransa, 686 hivi) alikuwa kwanza jambazi kutoka familia tajiri.

Baada ya kuongoka kwa msaada wa Autberi, akawa mmonaki, halafu abati wa monasteri alizoanzisha chini ya kanuni ngumu ya Kolumbani[1] [2][3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[4].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Juni[5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.