Lambati wa Vence

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yenye masalia yake katika kanisa kuu la Vence.

Lambati wa Vence (jina la kiraia kwa Kifaransa: Lambert Pelloquin; Bauduen, 1084 - Vence, 26 Mei 1154) alikuwa askofu wa mji huo, leo nchini Ufaransa, tangu mwaka 1114. Kabla ya hapo alikuwa mmonaki huko Lerins tangu umri wa miaka 16[1].

Anakumbukwa kwa kusaidia maskini, aliowajengea hospitali ya kwanza mjini, na kwa kupenda kuishi kifukara[2][3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Mei[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.