Kungwi (ndege)
Kungwi | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kungwi madoa (Bubo africanus)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Kungwi ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Striginae katika familia Strigidae. Spishi fulani zinaitwa kokoko. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi na spishi za jenasi Bubo ni miongoni mwa spishi kubwa kabisa za Strigidae.
Kungwi wana mgongo kwa rangi ya kahawa au kijivu pamoja na madoa meupe, na mbele yao ni nyeupe pamoja na madoa au michirizi nyeusi au kahawia. Spishi nyingi zina vishungi viwili vya manyoya vinavyofanana na masikio
Ndege hawa hula mamalia wadogo na wakubwa kiasi hasa (mpaka paa mdogo) lakini ndege, watambaazi na wadudu pia. Kokoko-walasamaki hula samaki hasa. Huwinda usiku.
Kwa kawaida jike huyataga mayai 2 lakini 1-5 inawezekana. Tago lao ni ardhini, mitini, kwenye miamba iliyojitokeza nje na hata kwenye vishubaka vya madirisha.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Bubo africanus, Kungwi Madoa (Spotted eagle-owl)
- Bubo ascalaphus, Kungwi-jangwa (Pharaoh eagle-owl)
- Bubo bubo, Kungwi wa Ulaya (Eurasian eagle-owl)
- Bubo b. hispanus, Kungwi wa Hispania (Iberian eagle-owl) - imekwisha sasa katika Afrika
- Bubo capensis, Kungwi Kusi (Cape eagle-owl)
- Bubo c. capensis, Kungwi wa Afrika ya Kusini (Southern African eagle-owl)
- Bubo c. mackinderi, Kungwi wa Mackinder (Mackinder's eagle-owl)
- Bubo c. dilloni, Kungwi wa Afrika ya Kaskazini (Northern African eagle-owl)
- Bubo cinerascens, Kungwi Kijivu (Greyish eagle-owl)
- Bubo lacteus, Kokoko (Verreaux's eagle-owl)
- Bubo leucostictus, Kungwi wa Akun (Akun eagle-owl}
- Bubo poensis, Kungwi wa Fraser (Fraser's eagle-owl)
- Bubo shelleyi, Kungwi wa Shelley (Shelley's eagle-owl)
- Bubo vosseleri, Kokoko wa Usambara (Usambara eagle-owl)
- Jubula lettii, Kungwi Manyoya-marefu (Maned owl)
- Scotopelia bouvieri au Bubo bouvieri, Kokoko-mlasamaki Michirizi (Vermiculated fishing owl)
- Scotopelia peli au Bubo peli, Kokoko-mlasamaki Madoa (Pel's fishing owl)
- Scotopelia ussheri au Bubo ussheri, Kokoko-mlasamaki Mwekundu (Rufous fishing owl)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Bubo bengalensis (Indian au Rock eagle-owl)
- Bubo blakistoni au Ketupa blakistoni (Blakiston's fish owl)
- Bubo coromandus (Dusky eagle-owl)
- Bubo magellanicus (Lesser au Magellanic horned owl)
- Bubo nipalensis (Spot-bellied eagle-owl)
- Bubo philippensis (Philippine eagle-owl)
- Bubo scandiacus Snowy owl)
- Bubo sumatranus (Barred eagle-owl)
- Bubo virginianus (Great horned owl)
- Ketupa flavipes au Bubo flavipes {Tawny fish owl)
- Ketupa ketupu au Bubo ketupu {Buffy fish owl)
- Ketupa zeylonensis au Bubo zeylonensis (Brown fish owl)
- Lophostrix cristata (Crested owl)
- Pulsatrix koeniswaldiana (Tawny-browed owl)
- Pulsatrix melanota (Band-bellied owl)
- Pulsatrix perspicillata (Spectacled owl)
Spishi za kabla ya historia
[hariri | hariri chanzo]- Bubo binagadensis (Mwisho wa Pleistocene ya Binagady, Azerbaijan)
- Bubo florianae (Mwisho wa Miocene}
- Bubo leakeyae (Mwanzo wa Pleistocene ya Tanzania)
- Bubo osvaldoi Cuban Horned Owl, (Mwisho wa Pleistocene ya Kuba)
- Bubo sp. (Mwisho wa Pliocene ya Senèze, Ufaransa)
- Bubo sp. (Mwisho wa Pliocene ya Rębielice Królewskie, Poland)
- Bubo sp. (Mwisho wa Pleistocene ya San Josecito Cavern, Mexiko)
- Pulsatrix arredondoi (Mwisho wa Pleistocene ya Cueva de Paredones, Kuba)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kungwi-jangwa
-
Kungwi wa Ulaya
-
Kungwi kusi
-
Kungwi kijivu
-
Kokoko
-
Kokoko-mlasamaki madoa
-
Rock eagle-owl
-
Blakiston's fish owl
-
Dusky eagle-owl
-
Lesser horned owl
-
Spot-bellied eagle-owl
-
Pilippine eagle-owl
-
Snowy owl
-
Barred eagle-owl
-
Great horned owl
-
Tawny fish owl
-
Buffy fish owl
-
Brown fish owl
-
Crested owl
-
Tawny-browed owl
-
Band-bellied owl
-
Spectacled owl