Kokoko-mlasamaki
Kokoko-mlasamaki | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Kokoko-walasamaki ni ndege mbuai wa jenasi Ketupa na Scotopelia katika familia Strigidae. Siku hizi wataalamu wengi wanawaainisha katika jenasi Bubo. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi na wana mnasaba na kungwi.
Ndege hawa wana mgongo kwa rangi ya kahawa au kijivu pamoja na madoa meupe, na mbele yao ni nyeupe pamoja na madoa au michirizi nyeusi au kahawia. Spishi za Ketupa zina vishungi viwili vya manyoya vinavyofanana na masikio.
Kokoko-walasamaki wanatokea karibu na mito na maziwa katika misitu minene. Huwinda usiku na hula samaki hasa lakini amfibia na wanyama wadogo pia.
Jike huyataga mayai 1 au 2 lakini mara nyingi kinda moja aishi tu. Kwa kawaida tago lao ni kwenye mti mkubwa lakini katika shimo la mwamba pia.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Scotopelia bouvieri au Bubo bouvieri, Kokoko-mlasamaki Michirizi (Vermiculated Fishing-owl)
- Scotopelia peli au Bubo peli, Kokoko-mlasamaki Madoa (Pel's Fishing-owl)
- Scotopelia ussheri au Bubo ussheri, Kokoko-mlasamaki Mwekundu (Rufous Fishing-owl)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Ketupa blakistoni au Bubo blakistoni (Blakiston's Fish )wl)
- Ketupa flavipes au Bubo flavipes {Tawny Fish Owl)
- Ketupa ketupu au Bubo ketupu {Buffy Fish Owl)
- Ketupa zeylonensis au Bubo zeylonensis (Brown Fish Owl)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Blakiston's fish owl
-
Tawny fish owl
-
Buffy fish owl
-
Brown fish owl