Kuhani
Kuhani ni mtu ambye katika dini nyingi, anashika nafasi ya mshenga kati ya Mungu (au miungu, mizimu n.k.) na binadamu wenzake.
Kuhani katika Biblia
[hariri | hariri chanzo]Katika Biblia ya Kiebrania anaitwa כּהן (kôhên), neno lililotafsiriwa katika Kigiriki kwa neno ἱερεύς (hiereus).
Ukuhani ulikuwa haki na wajibu wa wanaume wa kabila la Lawi tu, hasa ukoo wa Haruni, aliyewekwa wakfu na mdogo wake, Musa, mwanzoni mwa taifa la Israeli.
Umuhimu wake ulitegemea hekalu, altare na sadaka. Hivyo kuanzia mwaka 70 B.K., lilipobomolewa hekalu la Yerusalemu, lililokuwa pekee katika dini ya Uyahudi, makuhani wakakosa kazi hadi leo.
Ukristo, kwa kutegemea hasa Waraka kwa Waebrania, unamkiri Yesu kuwa ndiye kuhani wa milele anayetoa huduma yake kwa ajili ya watu akiwa katika hekalu la mbinguni.