Kristofa wa Collesano
Mandhari
(Elekezwa kutoka Kristofa na Kali)
Kristofa wa Collesano (Collesano, Sicilia, karne ya 9 - Basilicata, 981) alikuwa baba wa familia tajiri ambaye alijitosa pamoja na mke wake Kali na watoto wao wawili, Saba na Makari, kueneza umonaki wa Ukristo wa Mashariki[1].
Kwanza alijiunga na monasteri ya Wabazili akaruhusiwa kuishi kama mkaapweke halafu akafikiwa na mke na watoto wakAsaidiana naye kueneza umonaki huo katika sehemu mbalimbali za Italia Kusini iliyozidi kuvurugwa na wavamizi Waislamu[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, sawa na familia yake yote.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Desemba[3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Lynn White Jr. "The Byzantinization of Sicily." The American Historical Review. Vol. 42, No. 1 (Oct., 1936). p. 5.
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/81960
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
.