Rasi ya Kola
Rasi ya Kola (kwa Kirusi Ко́льский полуо́стров kolsky poluostrov) ni rasi iliyoko kaskazini magharibi mwa Urusi. Sehemu kubwa ya maeneo ya Obmansk Oblast iko humo. [1] Eneo la rasi ni km2 100000, linganisha Murmansk Oblast jumla km2 144900.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Rasi iko kabisa ndani ya mzingo aktiki ikipakana na Bahari ya Barents upande wa kaskazini na Bahari Nyeupe pande za mashariki na kusini-mashariki. Jiji la Murmansk ndilo mji mkubwa wenye wakazi zaidi ya 300,000 ambao ni wengi kwenye rasi.
Rasi hii ni baridi mno kwa kilimo ilikaliwa na wawindaji na Wasami waliofuga kulungu aktiki (reindeer). Tangu karne ya 12 Warusi kutoka Novgorod walianza kufika na rasi ilikuwa chini ya mamlaka ya milki za Warusi. Walivutwa na bahari yenye uvuvi bora; ingawa Kola iko upande wa kaskazini wa mzingo aktiki, bahari yake haina barafu ya kudumu kwa sababu mkondo wa ghuba kutoka Atlantiki unaendelea kupeleka maji ya vuguvugu hadi huko. Katika maji hayo samaki mbalimbali wanapatikana kwa wingi.
Katika kipindi cha Umoja wa Kisovyeti uchimbaji wa madini ulipanuka pamoja na tasnia za uvuvi na ufugaji wa kulungu aktiki. Idadi ya wakazi iliongezeka sana.
Bandari za rasi zilikuwa vituo muhimu kwa wanamaji wa jeshi la Kisovyeti. Bandari kuu ni Murmansk.
Baada ya kufsambaratika kwa Umoja wa Kisovieti, uchumi ulirudi nyuma na idadi ya watu ikaanza kupungua haraka. Kati ya 1989 na 2002, Obmansk Oblast ilipoteza karibu robo ya wakazi wake. Lakini uchumi uliibuka kwa kiasi fulani katika muongo wa kwanza wa miaka ya 2000 na rasi bado ndio eneo linaloonyesha maendeleo kati ya miji ya kaskazini ya Urusi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 2007 Atlas of Murmansk Oblast, p. 2
Marejo mengine
[hariri | hariri chanzo]- Министерство транспорта Российской Федерации. Федеральное агенство геодезии и картографии (2007). Мурманская область. Атлас. Санкт-Петербург: ФГУП "Геодезия".
- Главное управление геодезии и картографии при Совете Министров СССР. Научно-исследовательский географо-экономический институт Ленинградского государственного университета имени А. А. Жданова (1971). Атлас Мурманской области. Москва.
{{cite book}}
: CS1 maint: location missing publisher (link) - Бартольд Е. Ф. (1935). По Карелии и Кольскому полуострову. ОГИЗ/Физкультура и туризм.
- Wm. O. Field, Jr. The Kola Peninsula. Gibraltar of the Western Arctic. The American Quarterly on the Soviet Union. July 1938. Vol. I, No. 2.
- Жиров Д. В., Пожиленко В. И., Белкина О. А. и др. (2006). Терский район (tol. la 2-е, испр. и доп.). Ника.
{{cite book}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - Simon Richmond (2006). Russia & Belarus. Lonely Planet. ISBN 9781741042917. Iliwekwa mnamo 2010-01-21.
- Rudolf Avenhaus; na wenz. (2002). Containing the Atom. Oxford: Lexington Books. ISBN 9780739103876. Iliwekwa mnamo 2010-01-20.
- Olga Rigina. GIS Analysis of Surface Water Chemistry Susceptibility and Response to Industrial Air Pollution in the Kola Peninsula, Northern Russia. Published in Biogeochemical Investigations at the Watershed, Landscape, and Regional Scales, Springer 1998.
- Архивный отдел Администрации Мурманской области. Государственный Архив Мурманской области. (1995). Административно-территориальное деление Мурманской области (1920–1993 гг.). Справочник. Мурманск: Мурманское издательско-полиграфическое предприятие "Север".
- Michael P. Robinson; Karim-Aly S. Kassam (1998). Sami potatoes: living with reindeer and perestroika. Calgary: Bayeux Arts. ISBN 9781896209111. Iliwekwa mnamo 2010-01-20.
- Kigezo:Cite Soviet law
- Galina Ivanova (2000). Donald J. Raleigh (mhr.). Labor Camp Socialism: The Gulag in the Soviet Totalitarian System. M. E. Sharpe, Inc. ISBN 9780765639400. Iliwekwa mnamo Septemba 24, 2012.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Mikhail Kozlov; na wenz. (2009). Impacts of Point Polluters on Terrestrial Biota: Comparative Analysis of 18 Contaminated Areas. Springer. ISBN 9789048124671. Iliwekwa mnamo Januari 21, 2010.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - А. Е. Ферсман (1941). Полезные ископаемые Кольского полуострова. Москва, Ленинград: Издательство Академии наук СССР.
- Jane Costlow; Amy Nelson (2010). Other Animals: Beyond the Human in Russian Culture and History. Pittsburgh: University of Pittsburgh Press. ISBN 9780822960638. Iliwekwa mnamo 2010-01-20.
- Kigezo:RussiaBasicLawRef
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- media kuhusu Kola Peninsula pa Wikimedia Commons
Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Kola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |