Nenda kwa yaliyomo

Kofi Annan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Koffi Annan)
Kofi Annan (2003)

Kofi Atta Annan (8 Aprili 1938 - 18 Agosti 2018) alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa 1996 - 2006. Annan na Umoja wa Mataifa walipata Tuzo ya Amani ya Nobeli mwaka 2001. Alikuwa mwanzilishi na mwenyekiti wa Kofi Annan Foundation na pia mwenyekiti wa Elders, shirika la kimataifa lililoanzishwa na Nelson Mandela.

Alizaliwa huko Kumasi, Ghana. Alipewa jina Kofi kuonyesha kuwa alizaliwa siku ya Ijumaa kuendana na utamaduni wa Ashanti. Jina Annan linamaanisha kuwa alikuwa ni mtoto wa nne kuzaliwa.

Annan alienda shule ya Mfantsipim katika mji wa Cape Coast, Ghana (1954-1957). Baadaye, alienda Kumasi shule ya sayansi na teknolojia (sasa ni Kwame Nkruma Shule ya sayansi na teknolojia) kwa mwaka mmoja. Msaada kutoka Taasisi ya Ford ulimwezesha kusoma uchumi katika chuo kikuu cha Macalester, Saint Paul, Minnesota. Alipomaliza shahada ya kwanza mwaka 1961, alisoma mahusiano ya kimataifa katika chuo kikuu cha kimataifa masomo katika Geneva, Switzerland (1961-62). Alisoma katika chuo kikuu cha MIT, shule ya Sloan, na alipata shahada ya M.S.

Mtumishi wa Umoja wa Mataifa

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya masomo ya uchumi alijiunga na huduma ya Umoja wa Mataifa mwaka 1962 katika WHO. 1974-1976 alifanya kazi Ghana halafu akarudi tena huduma ya UM. Akapanda ngazi kuwa Makamu wa Katibu Mkuu mhusika wa usalama aliwajibika kusimamia shughuli za wanajeshi walio chini ya UM.

Alihusika na vita ya Rwanda pia ya Yugoslavia ambako wanajeshi chini ya bendera ya UM walishirikiana.

Katibu Mkuu

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1996 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UM, akarudishwa cheo mwaka 2001. Tangu 1 Januari alifuatwa ofisini na Ban Ki-moon.

Mpatanishi nchini Kenya

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2008 Annan alirudi katika habari za kimataifa alipofika Kenya kwa shabaha ya kupatanisha viongozi wa kisiasa waliopigana juu ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa Kenya 2007. Akisaidiana na Grace Machel na rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliendesha majadiliano kati ya wawakilishi wa ODM na PNU kwa muda wa wiki 5. Akafaulu kuleta mapatano ya ushirikiano kati ya pande zote mbili.

Maisha ya binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Kofi Annan ameoa mara ya pili. Mke wake Nane Maria Annan anatoka Uswidi. Ana watoto watatu.