Klementi na Agatanjelo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Klementi.
Picha takatifu ya Mt. Agatanjelo.

Klementi na Agatanjelo (walifariki Ankara, Uturuki ya leo, 312) walikuwa askofu wa Ankara na shemasi wake aliyemfuata kutoka Roma.

Walipata kuwa wafiadini wa Kikristo chini ya kaisari Diokletian ambaye alijaribu kumfanya Klementi aasi hata kwa mateso makali sana. Hatimaye waliuawa kwa kukatwa kichwa na askari wakati walipokuwa wanaadhimisha Liturujia ya Kimungu[1]

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi, na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 23 Januari[2] au 5 Februari.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Serbian Orthodox Church The Hieromartyr Clement, Bishop of Ancyra (January 23rd)
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.