Nenda kwa yaliyomo

Kisuke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kisuke ni kata ya Wilaya ya Ushetu katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania.

Hadi mwaka 2015 kata ya Kisuke ilikuwa inajumuisha vijiji zaidi ya 12 ambavyo ni: Kisuke, Kalaba, Nyamilangano, Bukomela, Nussa, Ngokolo, Mitonga, Mapamba, Kawekunelela, Itumbo, Kalaba na Ipilinga.

Baada ya hapo kata hiyo kubwa iligawanywa na kutengeneza kata nne yaani: Kisuke, Nyamilangano, Bukomela na Mapamba. Kata ya Kisuke imebaki na vijiji vinne tu: Kisuke (makao makuu ya kata), Itumbo, Kalaba na Ipilinga.

Idadi ya wakazi

[hariri | hariri chanzo]

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 6,152 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,467 waishio humo.[2]

Wakazi wengi wa kata hii ni Wakristo na Waislamu, huku idadi ndogo ya watu wakiwa hawana dini yoyote.

Eneo la kihistoria

[hariri | hariri chanzo]

Kata ya Kisuke iliwahi kutembelewa na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julius K. Nyerere, mnamo mwaka 1973 alipofanya uzinduzi wa Ofisi ya CCM kata ya Kisuke ambayo mpaka leo ipo na inaendelea kutumika.

Kata ya Kisuke ina Shule za msingi mbili: Shule Ya Msingi Kisuke na Shule Ya Msingi Itumbo. Pia kuna mradi wa kujenga shule nyingine mbili katika vijiji vya Ipilinga na Kalaba.

Huduma za afya

[hariri | hariri chanzo]

Kata ina vituo vya afya viwili: kimoja katika senta ya Kisuke kilichojengwa mwanzoni mwa miaka ya 1990 na kingine katika kijiji cha Itumbo katika kitongoji cha Magereza.

Wakazi wa kata ya Kisuke wanajishughulisha sana na kilimo na ufugaji.

Kati ya wazee mashuhuri wa kata hii kuna Nyahinga Katumbati, mfugaji wa nyuki mkubwa, John Lutonja, Bulyankulu Ng'ombejanke, mfugaji katika kijiji cha Itumbo, na Athumani Mabumba, mjasiriamali katika kijiji hichohicho.

Biashara

[hariri | hariri chanzo]

Kata ina magulio mawili: gulio la Kisuke lililopo katika mtaa wa Mji Mwema, kijiji cha Kisuke, na gulio la Itumbo lililopo katika mtaa wa Senta, kijiji cha Itumbo.

Kata za Wilaya ya Ushetu - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania

Bukomela * Bulungwa * Chona * Chambo * Igunda * Idahina * Kinamapula * Igwamanoni * Kisuke * Mapamba * Mpunze * Nyamilangano * Nyankende * Sabasabini * Ubagwe * Ukune * Ulewe * Ushetu * Ulowa * Uyogo

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kisuke kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.