Nyankende

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyankende ni kata ya Wilaya ya Ushetu katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 20,078 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,515 waishio humo [2].

Kata ya Nyankende ilifanikiwa kuwa na zahanati mwaka 2014 ambapo ilijengwa katika kijiji cha Nyankende. Pia kijiji cha Bunanda mwaka 2016 kilianzishiwa zahanati ya pili kuleta jumla ya zahanati 2 katika kata.

Mwaka 2015 kata iliweza kupata shule moja ya sekondari iliyopewa jina la Nyankende huku wakianza na walimu saba tu ikiwemo wawili wa sayansi na watano wa masomo ya sanaa; mbali na hilo ina shule za msingi sita: 1. Nyankende 2. Bunanda 3. Sinwankere 4. Kagera 5. Akzyoba na 6. Nyambeshi.

Kwa kumalizia kuna miradi mikuu miwili: wa kwanza ni maji na wa pili umeme ambao bado utekelezaji haujaanza

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Ushetu - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania

Bukomela * Bulungwa * Chona * Chambo * Igunda * Idahina * Kinamapula * Igwamanoni * Kisuke * Mapamba * Mpunze * Nyamilangano * Nyankende * Sabasabini * Ubagwe * Ukune * Ulewe * Ushetu * Ulowa * Uyogo

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyankende kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.