Kiolwa cha anga-nje
Jump to navigation
Jump to search
| |||||||
Mifano ya violwa vya angani |
Kiolwa cha anga-nje (pia: gimba la angani, kwa Kiingereza: astronomical object au celestial body) ni jina la jumla kwa ajili ya vitu vinayopatikana katika anga ya ulimwengu.
Kati ya vitu hivyo huhesabiwa:
- Jua
- Sayari
- Sayari kibete
- Miezi
- Vimondo (pia meteori au meteroidi)
- Asteroidi
- Nyotamkia
- Nyota
- Galaksi
- Nebula
- Mawingu katika anga
Hivyo vyote ni violwa asilia. Vitu vilivyoko kwenye anga-nje vilivyotengenezwa na binadamu ni vyombo vya anga-nje. Hapa kuna swali kama mabaki kutokana na vyombo vya anga-nje vilivyovunjika au takataka zinazotokana na safari za anga-nje yanastahili kuitwa kwa neno hili.
Elimu ya violwa vya anga-nje ni astronomia.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiolwa cha anga-nje kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |