Nenda kwa yaliyomo

Nebula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
picha ya Nebula NGC 604 katika galaksi M33 iliyoko na umbali wa miakanuru milioni 2.7 kutoka dunia yetu. Hili ni eneo ambako nyota mpya zinazaliwa

Nebula ni neno linalotumika kwa ajili ya kutaja eneo angavu na jeupejeupe linaloonekana angani ama kwa macho au kwa darubini.

Zamani hata galaksi ziliweza kuitwa "nebula". Galaksi ya Andromeda iliyokuwa galaksi ya kwanza kutambuliwa angani ilikuwa inaitwa "Andromeda Nebula".

Siku hizi neno linataja wingu kubwa linalong'aa. Maada yake inaweza kuwa gesi ya moto, vumbi na utegili.

Gesi ya moto na utegili zinang'aa pekee yake; vumbi linaweza kuakisi nuru ya nyota za karibu.

Mara nyingi nebula ni mahali pa kuzaliwa au kutokea kwa nyota mpya. Wakati mwingine wingu ni mabaki tu ya nyota aina ya nova, yaani nyota iliyokufa katika mlipuko mkubwa.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nebula kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.