Mwaka wa nuru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwaka wa nuru ni kipimo cha umbali kinachotumiwa katika fani ya astronomia. Kinataja umbali unaopitiwa na nuru ikitembea kwa muda wa mwaka mmoja wa dunia yaani siku 365.25.[1]

Msingi wa kipimo hiki ni kasi ya nuru. Nuru inatembea takriban kilomita 300,000 kwa sekunde. Idadi kamili ni mita 299,792,458 kwa sekunde moja. Mwezi wa dunia yetu una umbali na dunia yetu kama sekunde moja ya nuru au kilomita lakhi tatu na dunia.

Katika mwaka mmoja umbali huo unafika mita 9.461  × 1015.

Kipimo hiki kinahitajika kutaja umbali kati ya nyota na nyota angani. Umbali huu umepimwa kuwa miaka ya nuru mamia, maelfu au hata mamilioni. Kutokana na ukubwa wa ulimwengu umbali katika anga ni kubwa sana. Nyota jirani kabisa na jua letu inaitwa Alpha Centauri umbali wake ni 4.2 miaka ya nuru maana yake nuru yake inahitaji zaidi ya miaka minne hadi imefika kwetu. Kwa maana nyingine tunaiona nyota hii jinsi ilivyoonekana miaka minne iliyopita.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Measuring the Universe The IAU and astronomical units, Tovuti ya Ukia, iliangaliwa Julai 2017