Kimetameta (kisubi)
Kimetameta | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kimetameta wa Nyuzilandi (Arachnocampa luminosa)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Jenasi 3:
|
Vimetameta au vimulimuli ni lava wa visubi-kuvu wa familia Keroplatidae wanaotoa nuru (bio-uangazaji). Majina hayo yanaweza kutumiwa pia kutaja spishi za mbawakawa za familia ya juu Elateroidea. Visubi hao huitwa visubi-kuvu kwa sababu angalau sehemu ya chakula chao ni vikungunyanzi na spora za kuvu. Nuru wanayotoa ina shughuli ya kuvutia wadudu wengine wadogo. Vimetameta hao hawapatikani katika Afrika.
Lava wa jenasi tatu za visubi-kuvu huonyesha bio-uangazaji. Wanatoa nuru kijanibuluu[1]. Wanasuka tando zinazonata ili kukamata wadudu wadogo. Hupatikana katika mapango na mashimo ya miamba, chini ya miamba inayotokeza na katika mahali pengine panyevu panapokingwa. Licha ya lingano kwa shughuli na muonekano, mifumo ya bio-uangazaji ya jenasi tatu sio ya aina moja na inaaminika kuwa iligeuka kwa jinsi tofauti[2][3][4].
- Jenasi Arachnocampa: spishi tano zinazopatikana tu katika Nyuzilandi na Australia. Mwanajenasi anayejulikana sana ni kimetameta wa Nyuzilandi, Arachnocampa luminosa. Lava ni mbuai na hutumia nuru yao kuchua mbuawa katika tando zao.[5].
- Jenasi Orfelia: ina spishi moja tu, Orfelia fultoni, inayopatikana tu katika Amerika ya Kaskazini. Kama spishi za Arachnocampa lava wake hutumia nuru yao kuvutia wadudu mkia-fyatuo na wadudu wengine wadogo, lakini chakula chao kikuu ni spora za kuvu.
- Jenasi Keroplatus: inapatikana huko Eurasia. Kinyume na Arachnocampa and Orfelia, lava wa Keroplatus hujilisha kwa spora za kuvu tu[6]. Bio-uangazaji yao inaaminika kutokuwa na shughuli na ni mabaki[2].
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Vimetameta vivwili vya Nyuzilandi (Arachnocampa luminosa) katika Waitomo Caves
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Vadim Viviani. "Terrestrial Bio luminescence: Biological and Biochemical Diversity". Photobiological Sciences Online. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 Yuichi Oba (2014). "Insect Bioluminescence in the Post-Molecular Biology Era". Katika Klaus H. Hoffmann (mhr.). Insect Molecular Biology and Ecology. CRC Press. uk. 94. ISBN 9781482231892.
- ↑ Vadim R. Viviani; J. Woodland Hastings; Thérèse Wilson (2002). "Two bioluminescent diptera: the North American Orfelia fultoni and the Australian Arachnocampa flava. Similar niche, different bioluminescence systems". Photochemistry and Photobiology. 75 (1): 22–27. doi:10.1562/0031-8655(2002)075<0022:TBDTNA>2.0.CO;2. PMID 11837324.
- ↑ Lisa M. Rigby; David J. Merritt (2011). "Roles of biogenic amines in regulating bioluminescence in the Australian glowworm Arachnocampa flava". Journal of Experimental Biology. 214 (19): 3286–3293. doi:10.1242/jeb.060509. PMID 21900476.
- ↑ Meyer-Rochow, Victor Benno (2007). "Glowworms: a review of "Arachnocampa" spp and kin". Luminescence. 22 (3): 251–265. doi:10.1002/bio.955. PMID 17285566.
- ↑ Osawa, K; Sasaki, T; Meyer-Rochow, VB (2014). "New observations on the biology of Keroplatus nipponicus Okada 1938 (Diptera; Mycetophiloidea; Keroplatidae), a bioluminescent fungivorous insect". Entomologie Heute. 26: 139–149.