Nenda kwa yaliyomo

Kilongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kilongo ni lugha ya Kibantu inayotumiwa na Walongo wanaopatikana katika Mkoa wa Geita. Kilongo hutazamwa kama lahaja ya Kihaya.

Ni lugha inayofanana sana na Kinyambo, Kihaya, Kiganda, Kinyankole, Kizinza, Kikara na Kisubi: hii ni kwa sababu Walongo asili yao ni Wahaya, Wanyambo, Watutsi, Wanyankole na Waganda waliohamia Geita kukwepa vita na mauaji ya mapacha yaliyokuwa yakifanyika katika tamaduni za himaya ya Bunyoro ambapo mapacha waliitwa Abalongo na pacha aliitwa Omulongo. Kazi zao zilikuwa uhunzi wa vyuma, ufugaji, uwindaji na kilimo.

Walihamia Geita miaka mingi iliyopita na kuunda jamii ya Walongo ambao kwa sasa wamechanganyikana sana na Wasukuma kutokana na uhamiaji wa Wasukuma wengi katika mji wa Geita.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kilongo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.