Kilimarondo
Kilimarondo ni kata ya Wilaya ya Nachingwea katika mkoa wa Lindi, Tanzania yenye msimbo wa posta namba 65326[1].
Kata hiyo ina jumla ya vijiji vitatu ambavyo ni Namatunu, Nanjihi na Kilimarondo.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, idadi ya wakazi wa kata ilikadiriwa kuwa watu 4,509.[2]
Asilimia kubwa ya wakazi wa kata ya Kilimarondo ni Wandonde, kabila ambalo lugha yake ya asili inaelekea kupotea katika uso wa dunia.
Shughuli kubwa ya uchumi kwa wakazi wa Kilimarondo ni kilimo cha mazao mchanganyiko.
Kilimarondo pia kuna parokia ya Kanisa Katoliki ndani ya Jimbo Katoliki la Lindi. Parokia hiyo ilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1940 na wamisionari Wazungu.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ https://tcra.go.tz/services/publication-of-postcode-list Tanzania Postcode List
- ↑ Makadirio ya Idadi ya Watu katika Majimbo ya Uchaguzi kwa Mwaka 2016, Tanzania Bara, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dar es Salaam April 2016, iliangaliwa Mei 2021
![]() |
Kata za Wilaya ya Nachingwea - Mkoa wa Lindi - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Boma | Chiola | Kiegei | Kilimani Hewa | Kilimarondo | Kipara Mnero | Kipara Mtua | Lionja | Marambo | Matekwe | Mbondo | Mchonda | Mitumbati | Mkoka | Mkotokuyana | Mnero Miembeni | Mnero Ngongo | Mpiruka | Mutua | Nachingwea Mjini | Naipanga | Naipingo | Namapwia | Namatula | Nambambo | Namikango | Nang'ondo | Nangowe | Nditi | Ndomoni | Ngunichile | Ruponda | Stesheni | Ugawaji |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kilimarondo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |