Nenda kwa yaliyomo

Kifo Cheusi Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Uingereza.
Kifo Cheusi Uingereza

Kifo Cheusi ilikuwa jina la pandemia ya ugonjwa wa tauni (kwa Kiingereza: bubonic plague) ambao uliwahi kuingia nchini Uingereza mnamo mwezi Juni 1348. Ilikuwa miongoni mwa dalili za awali za pandemia ya pili, iliyosababishwa na bakteria wa Yersinia pestis. Istilahi Kifo Cheusi haikutumika mpaka mwishoni mwa karne ya 17.

Asili au chanzo cha ugonjwa huu ni Bara la Asia, ila ulienea upande wa magharibi kipindi cha misafara ya biashara zilizozunguka Ulaya na uliwasili katika taifa la Uingereza Kusini-Magharibi kutoka kwenye jimbo la Gascony.

Ugonjwa huo wa tauni ulienezwa kwa kuambukizwa kupitia panya (flea-infected rats), vivyo hivyo pamoja na watu walioathiriwa na ugonjwa huo, panya walikuwa ni vekta wa Bakteria aina ya Yersinia pestis na Oriental rat flea walikuwa ni vekta wa awali.

Kisa cha kwanza kugundulika Uingereza kilikuwa cha baharia aliyewasili katika mji wa Weymouth, Dorset, kutoka Gascony mnamo mwezi juni 1348. Wakati wa kiangazi, ugonjwa wa tauni ulifika London, na wakati wa kipupwe pia ulisambaa katika lango la kuingilia Uingereza mnamo mwaka 1349, kabla hauja punguza kasi ilipofika mwezi Disemba, makadilio ya kiwango cha chini cha idadi ya vifo mwanzoni mwa karne ya 20 viliongezeka zaidi kutokana na kurudiwa kwa ukusanyaji mpya wa taarifa, kwa kiasi cha asilimia 40–60 ya idadi kubwa ya watu ilikubalika.

Matokeo ya awali yalikuwa yakipelekea kampeni ya mapambano kwa miaka mia moja. Kwa kipindi kirefu idadi ya watu ilipungua na kusababisha uhaba wa wafanyakazi, pamoja na kufuatiwa kwa kuibuka kwa malipo ya posho, ilipingwa na wamiliki wa ardhi, ambayo ilisababisha chuki ya hali ya juu miongoni mwa tabaka la chini. Mapinduzi ya wakulima wadogo wadogo ya mwaka 1381 kwa ujumla yalipelekea chuki kubwa , na hata hivyo uasi ulitokomezwa kwa kipindi kirefu cha utawala wa Kikabaila na ulikwisha kabisa nchini Uingereza. Kifo Cheusi pia kiliathiri juhudi za sanaa na utamaduni, na ilisaidia kuongeza matumizi ya lugha za asili.

Miaka 1361–1362 Ugonjwa wa tauni ulirejea nchini Uingereza, kwa kipindi hicho ulisababisha vifo kufikia asilimia 20 ya idadi ya watu. Baada ya hapo Ugomjwa wa tauni uliendelea kurejea kwa vipindi mpaka karne ya 14 na 15, kwa matokeo ya vijiji mpaka taifa zima kwa ujumla. Kufuatiwa na athari zake kwa uchache pamoja na mojawapo ya matokeo ya mwisho ya ugonjwa wa tauni nchini Uingereza ilikuwa ni ugonjwa wa tauni wa miaka 1665–1666 jijini London.

Jina la "Black Death"

[hariri | hariri chanzo]

Jina la kifo cheusi (black death) halikutumiwa bado wakati wa awamu ya kwanza ya ugonjwa huo. Wakati ule vyanzo vya kimaandishi yaliyohifadhiwa yalitumia majina kama "Great Pestilence" au "Great Mortality"[1]. Wakati wa awamu ya pili ya pandemia hiyo katika karne ya 17 jina la "kifo cheusi" lilianza kutumiwa, kutokana na matumizi yake pale nchi za Skandinavia[2]. Asili ya jina ni kutokea kwa doa nyeusi kwenye ngozi kutokana na kufa kwa seli chini ya ngozi zisizopata oksijeni ya kutosha shauri la athira ya ugonjwa.

Kwa ujumla leo hii inaeleweka kwamba ugonjwa huo, ambao haukuwa na jina mahususi au rasmi hapo awali, ulikuwa tauni, inayosababishwa na bakteria aina ya Yersinia pestis. Bakteria hawa hubebwa na viroboto wanaokaa kwenye panya. Wakati viroboto humdunga binadamu, bakteria zinazokaa ndani ya wadudu hao zinaingia katika damu na kufika kwenye tezi za limfu ambako zinaongezeka na kusababisha uvimbe. Kutoka hapa zinaenea hadi kufika wengu na mapafu. Wakati idadi kubwa ya bakteria inakufa mwilini, zinasababisha sumu kwenye damu ya mtu na kuleta mzungukohafifu damu hadi kumwua mtu. Mgonjwa anapata homa kali na kuwa mdhaifu na kwa kawaida wagonjwa hufariki baada ya siku chache[3]. Aina nyingine ya ugonjwa huo ni tauni ya mapafu ambako maambukizi hupitishwa moja kwa moja kutoka mtu hadi mtu kwa njia ya bakteria katika pumzi[4].

  1. https://www.oed.com/view/Entry/280254 Black Death, n, Oxford English Dictionary online, iliangaliwa Novemba 2020
  2. Ziegler, Philip (2003). The Black Death (News ed.). Sutton: Sutton Publishing Ltd. ISBN 0-7509-3202-3., uk 17-18
  3. Horrox, Rosemary (1994). The Black Death. Manchester: Manchester University Press. ISBN 0-7190-3497-3., uk 5-6
  4. Byrne, J. P. (2004). The Black Death. London: Greenwood Publishing Group. ISBN 978-0-313-32492-5., uk 21-29
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kifo Cheusi Uingereza kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.