Kibondo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kibondo
Nchi Tanzania
Mkoa Kigoma
Wilaya Kibondo
Idadi ya wakazi
 - 25,570

Kibondo ni mji mdogo na makao makuu ya wilaya ya Kibondo katika Mkoa wa Kigoma (Tanzania). Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa kata ya Kibondo mjini ilihesabiwa kuwa 25,570 [1]. Mji uko kilomita 270 kazkazini ya Kigoma karibu na mpaka wa Burundi.

Wenyeji wa Kibondo ni hasa Waha.

Baada ya mapigano ya 1993 nchini Burundi wakimbizi wengi walifika Uha na kambi kubwa ilijengwa kando la mji wa Kibondo. Kambi hili lilikuwa na Waburundi 25,000 waliokuwa zaidi ya robo ya wakimbizi wote kutoka Burundi nchini Tanzania. Kambi hili lilileta biashara mjini lakini pia matatizo mbalimbali.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kibondo - Mkoa wa Kigoma - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bitare | Bunyanbo | Busagara | Busunzu | Itaba | Kibondo | Kitahana | Kizazi | Kumsenga | Mabamba | Misezero | Murungu | Rugongwe


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kigoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kibondo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.