Busagara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Busagara ni jina la kata ya Wilaya ya Kibondo katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 30,722 waishio humo.[1]

Vijiji[hariri | hariri chanzo]

Busagara ni kata iliyopo katika tarafa ya Kifura. Kata ina vijiji 4 kama vile Kifura, Kigendeka, Kasaka na Nyaruyoba.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa Busagara kilikuwa kijiji ambacho kilikuwa kikikaliwa na Waha wa mdyank'o (kaya) wa Washubhi na ilikuwa moja kati ya himaya ya mwami Luhaga aliyeitawala kibondo yote.

Baada ya uhuru 1961 wakazi walitakiwa kuishi katika vijiji vya ujamaa ndipo walipoanzisha kijiji cha Kasanda ambacho kwa sasa kinajulikana kama Kifura eneo ambao lililokuwa kijiji cha zamani cha Busagara kwa sasa ni mashamba .

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa Busagara ni wakulima hasa wa mazao ya chakula kama vile mahindi, mihogo, maharage ya njano, mtama, karanga, magimbi n.k.. Kilimo kinafanyika katika mashamba ya kunk'ubha, mrutunhu, busagara, mkugwa, kihivfu nyensato n.k.

Shule[hariri | hariri chanzo]

Kata ina shule za sekondari mbili za Moyowosi na Busagara. Asilimia kubwa ya wakazi ni maskini.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kibondo - Mkoa wa Kigoma - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bitare | Bunyanbo | Busagara | Busunzu | Itaba | Kibondo | Kitahana | Kizazi | Kumsenga | Mabamba | Misezero | Murungu | Rugongwe