Nenda kwa yaliyomo

Kibibimlima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kibibimlima
(Bellis perennis)
Kichwa cha maua cha kibibimlima
Kichwa cha maua cha kibibimlima
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Asterids (Mimea kama alizeti)
Oda: Asterales (Mimea kama alizeti)
Familia: Asteraceae (Mimea iliyo mnasaba na alizeti)
Nusufamilia: Asteroideae
Jenasi: Bellis
Spishi: B. perennis
L.

Kibibimlima (Bellis perennis) una asili yake katika Ulaya ya Magharibi, ya Kati na ya Kaskazini.

Mmea huo huwa na mizizi midogo inayomea ardhini lakini si kwa kuchimba sana ndani. Pia huwa na matawi madogo ya mviringo au matawi yenye kufanana kijiko yenye refi wa sentimita 2-5, ambayo hupatikana karibu sana na ardhi. Kichwa cha maua au kapitulo (capitulum) ni sentimita 2-3 kwa upana yakiwa. Viua vya ndani ni njano na vile vya nje ni vyeupe. Kibibimlima ni dikotiledoni.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Kibibimlima haathiriki na ukataji wa nyasi kwa hivyo yeye huwa kama mmea haribifu bustanini, ingawa wachache hupenda umbo la maua haya. Kuna aina za kibibimlima zinazopandwa kwa ajili ya kuuza, zenye maua makubwa zaidi yenye petali zenye upana wa sentimita 5-6

Maua yanatumika kimatibabu kwa sababu ya sifa zake za kufanya tishu za mwili kuwa ndogo.[1] Katika Roma ya kale, madaktari wa upasuaji waliofuata majeshi vitani waliwaamuru watumwa kukusanya magunia ya kibibimlima ili kupata kutoa maji kutoka maua yale.

Kibibimlima kimetumika tangu jadi kutengeneza vifaa vya kuremebsha katika michezo ya watoto.[2]

  1. Howard, Michael. Traditional Folk Remedies (Century, 1987), p129
  2. "Children's 'right to play'". BBC News. BBC. 2002-08-07. Iliwekwa mnamo 2008-11-02.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]