Kibaha Education Centre

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kibaha Education Centre (kifupi: KEC) ni taasisi ya elimu iliyoko Kibaha nchini Tanzania. Iko katika 6°47'22.2"S, 38°58'28.7"E katika halmashauri ya manispaa ya Kibaha.

KEC ilianzishwa mwaka 1963 chini ya ufadhili wa nchi tano, serikali ya Tanganyika (sasa Tanzania) kwa upande mmoja na nne ni Denmark, Finland, Norway na Sweden.Kabla ya kuikabidhi serikali ya Tanzania mwaka 1970, KEC ilijulikana kama mradi wa Nordic-Tanganyika mwaka 1961–1964.

Usimamizi[hariri | hariri chanzo]

KEC inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi inayojumuisha wawakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi,[1] Wizara ya Afya, Jumuiya ya Maendeleo, Jinsia, Wazee na watoto (MoHCDEC),[2] Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia (MoEST),[3] Wizara ya Fedha na mipango[4] na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), pamoja na wajumbe wengine watatu walioteuliwa na Bodi ya Wakurugenzi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]