Nenda kwa yaliyomo

Khartoum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Khartum)
Faili:Khartoumdowntown.jpg
Mji Wa Khartoum


Jiji la Khartoum
Jiji la Khartoum is located in Sudan
Jiji la Khartoum
Jiji la Khartoum

Mahali pa mji wa Khartoum katika Sudan

Majiranukta: 15°35′35″N 32°32′8″E / 15.59306°N 32.53556°E / 15.59306; 32.53556
Nchi Sudan
Majimbo Khartoum
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 2 090 001
Khartoum on map of Sudan
Msongamano wa magari kwenye kitovu cha Khartoum
Ramani ya Khartoum pamoja na Omdurman na Bahri
Picha ya angani ya Khartoum na Omdurman na Bahri
Mto Nile mbele ya Khartoum mnamo mwaka 1910
Mtaa mdogo wa Khartum

Khartoum (الخرطوم al-Khartūm) ni mji mkuu wa Sudan na pia mki mkuu wa dola la shirikisho la Khartoum. Mji uko mahali mito ya Nile nyeupe na Nile ya buluu inapokutana. Kisheria "Khartoum" ni eneo tu mashariki ya Nile nyeupe na kusini ya Nile ya buluu lakini hali halisi Khartoum pamoja na miji ya Omdurman na Bahri ni kama mji mmoja mkubwa sana unaounganishwa kwa madaraja kadhaa.

Khartoum ina wakazi 2,090,000 mjini penyewe pamoja na Omdurman na Bahri idadi ya wakazi inaweza kufika kati ya milioni 6 hadi 8 (kadirio la mwaka 2006).

Kuongezeka kwa idadai ya wakazi:

Mwaka Wakazi
(Khartoum penyewe)
Wakazi
(miji yote mitatu)
1956 93.100 245.800
1973 (sensa) 333.906 748.300
1983 (sensa) 476.218 1.340.646
1993 (sensa) 947.483 2.919.773
2006 (kadirio) 2.090.001 7.830.479

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Khartoum ilianzishwa mwaka 1820/21 na mtawala wa Misri Mehmed Ali kama kambi la jeshi mahali mito miwili ya Nile inapokutana. Wafanyabiashara wenyeji na Wamisri hawakuchelewa kujenga karibu. Kituo kipya ikawa kitovu cha biashara kwa ajili ya maeneo makubwa ya Sudan, hasa biashara ya meno ya ndovu, mpira wa miti, manyoya ya mbuni kwa ajili ya masoko ya Ulaya na watumwa kwa ajili ya masoko ya Misri, Uturuki na Uarabuni.

Sehemu kubwa ya karne ya 19 Khartoum ilikuwa na nyumba ndogo za udongo na mitaa nyembamba. Nyumba kubwa za pekee zilikuwa ikulu ya gavana wa Misri, msikiti mkuu, kanisa la Wakopti, misioni ya Wakatoliki tangu 1847 na nyumba kadhaa ya wafanyabiashara Wagiriki na wazungu wengine. Palikuwa na ofisi za kibalozi za Austria na Uingereza. Idadi ya wakazi ilifikia takriban 50,000 ambao wengi walikuwa Waarabu na watumwa Waafrika.

Wakati wa mtawala wa Misri Ismail Pascha Khartoum ikawa mji mkuu wa Sudan na makao ya gavana mkuu aliyekuwa Mwingerezea Gordon. Dhidi utawala wa Misri na Mwingereza Gordon kama gavana ilitokea ghasia na mapinduziy a Kiislamu. Jeshi la Muhammad Ahmad ibn Abd Allah Al-Mahdi iliteka Khartoum. Mahdi Muhammad hakutaka kukaa kwenye "mji wa makafiri" akajenga mji mpya wa Omdurman "mji wa waumini" ng'ambo ya mto Nile uliokuwa mji mkuu wa dola la mahdi 1885 - 1898.

Mwaka 1898 Waingereza chini ya jenerali Kitchener kwa kushirikiana na Wamisri walirudi Sudan na kumaliza utawala wa mahdi wakajenga Khartoum upya.

Historia ya kisasa

[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uhuru 1956 Khartoum ikawa mji mkuu wa Sudan huru.

Katika miaka tangu 1970 wakazi waliongezeka sana kutokana na wakimbizi waliokimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi za jirani kama Chad, Eritrea, Ethiopia na Uganda, pia wakimbizi kutoka vita ya Sudan ya Kusini. Wakimbizi hawa walijenga mitaa mikubwa ya vibanda.

Tar. 20. Agosti 1998 Khartoum ilisha,buliwa na ndege za kivita za Marekani kwa sababu Waamerika waliamini ya kwamba kiwanda fulani kilikuwa mahali pa kutengenezea silaha za kikemia kwa ajili ya Osama bin Laden. Imejulikana baadaye ya kwamba kiwanda hiki kilikuwa cha madawa tu, Marekani ilifaulu kuondoa uwezo wa Sudan wa kutengeneza Aspirin yake.

Mwaka 2005 viongozi wa Sudan ya Kusini waliweza kufika Sudan baada ya mapatano ya amani kati ya serikali ya Khartoum na Jeshi la ukombozi wa Sudan Kusini. Walipewa vyeo mbalimbali katika serikali mpya. Baada ya kifo cha kiongozi wa Sudan ya Kusini John Garang katika ajali ya ndege palitokea ghasia kali mwanzo wa Agosti 2005.


Maendeleo ya mji

[hariri | hariri chanzo]

Tangu mapatano ya amani kuhusu Sudan ya Kusini kuna mipango mikubwa ya kujenga kitovu kipya ya kibiashara kwa ajili ya Khartoum ni mradi wa "Al-Mogran". Kuna matumaini ya kwamba amani itawezesha nchi kutumia mapato kutokana na mafuta nchini kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Lakini wakati uleule vita ya jimbo la Darfur inaleta wasiwasi tena.

Khartoum ina vyuo vikuu vinne.


Makala hii kuhusu maeneo ya Sudan bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Khartoum kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.