Keyshia Cole
Keyshia Cole | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Keyshia Michelle Cole[1] |
Pia anajulikana kama | KC, The Princess of Hip-Hop Soul |
Amezaliwa | 15 Oktoba 1981 |
Aina ya muziki | R&B, hip-hop soul |
Kazi yake | Mwimbaji-mtunzi wa nyimbo |
Ala | Sauti |
Aina ya sauti | Soprano[2] |
Miaka ya kazi | 2004–hadi sasa |
Studio | A&M, Geffen |
Ame/Wameshirikiana na | Ron Fair, Manny Haley, Remy Ma, Monica, Daniel Gibson, Kanye West, Trina |
Tovuti | www.keyshiacole.com |
Keyshia Miesha Cole (amezaliwa tar. 15 Oktoba 1981)[2] ni msanii wa rekodi za muziki kutoka nchini Marekani. Ametoa albamu yake ya kwanza yenye platinum The Way It Is mnamo Juni 2005, na albamu yake aliyoitoa akiwa chuoni kwa mwaka wa pili iliyoitwa Just Like You hapo mwezi wa Septemba 2007. Albamu yake ya tatu, A Different Me ilitolewa mnamo tar. 16 Desemba 2008, nayo pia imetunukiwa platinum. Pia anajulikana kwa mfululizo wa makala ya tv Keyshia Cole: The Way It Is ambao inarushwa na TV ya BET kuanzia 2006 hadi 2008, kipindi ambacho kinaonesha uhusiano wa Keyshia kikazi na wazazi wake na ndugu pia.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Keyshia Cole alizaliwa mnamo tar. 15 Oktoba 1981 mjini Oakland, California, ambapo pia alikulia. Cole alizaliwa na Francine "Frankie" Lons na Sal ambaye ni marehe baba'ke. Baadaye akajakulelewa na Yvonne Cole na familia yake, marafiki wa Frankie, ambao ndiyo waliomlea. Akiwa pamoja na kaka Sean, Keyshia alianza kujionesha kwenye tasnia ya muziki tangu yungali na miaka 12, alikutana na kurekodi na MC Hammer.[3] Baadaye akaanzisha bendi na Tupac Shakur, ambaye alimwahidi kumsaidia kuanzisha kazi zake za uimbaji kabla hajafa kwa kutotarajia.[4] Baada ya kusimamisha uhusiano wake wa zahama, Cole akahamia mjini Los Angeles akiwa na umri wa miaka 18 akiwa na nia ya kujiendeleza zaidi kimuziki. Mwaka wa 2004, baada ya kutoka mixtape, alivutiwa sana na mtendaji mkuu wa A&M Records, Ron Fair,[5] ambaye aliingia naye mkataba na baadaye kuwa mshauri mkuu wake.
Shughuli
[hariri | hariri chanzo]2001-2005: Kabla ya The Way It Is
[hariri | hariri chanzo]Kabla hajaingia mkataba, Keyshia ameshirikiana na wasanii wale ambao wamezaliwa katika eneo moja la Bay Area, miongoni mwao ni D'Wayne Wiggins wa Tony Toni Tone na Messy Marv.
Katika matarajio yake ya albamu ya kwanza, Keyshia na DJ Green Lantern wakatoa mixtape, Team Invasion Presents Keyshia Cole, kunako mwezi wa Juni 2005. Imeshirikisha muuzo wa sura kama vile Shyne, Remy Ma, Fat Joe na Ghostface Killah. Mixtape imechukua biti ya nyimbo nyingi zilizorekodiwa na wasanii maarufu wa hip-hop kama vile 2Pac ("I Get Around"), Nas' ("Ether"), Mobb Deep ("Shook Ones (Part II)") na Scarface ("Guess Who's Back"). Vibao kama vile cha "(I Just Want It) To Be Over", ambayo ni remix ya "I Changed My Mind", na "I Should Have Cheated" navyo pia viliingizwa.
2004–2005: The Way It Is
[hariri | hariri chanzo]Single ya kwanza ya Keyshia ni "Never", ameshirikiana na Eve, ilitolewa mnamo tar. 23 Machi 2004 ili kusukuma kibwagizo cha filamu ya Barbershop 2: Back in Business. Single hii ilianguka kabisa kwenye chati, na Keyshia aliendelea kurekodi albamu yake ya kwanza kwa mwaka mzima wa 2004 hadi mwanzoni mwa mwaka wa 2005. "Never" hatimaye ikawa nyimbo ya mwisho kwenye orodha ya nyimbo za The Way It Is.
Mnamo tar. 9 Novemba 2004, Keyshia ametoa single ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "I Changed My Mind", akishirikiana na Kanye West. Single nafasi ya #71 nchini Marekani, na hakikuwa kibao kikali sana kwa Cole. Single ya pili kutoka katika albamu ni "(I Just Want It) To Be Over", ilitolewa mnamo tar. 5 Aprili 2005, na kufikia nafasi ya #1 kwenye chati Billboard Bubbling Under Hot 100 (#101).
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- The Way It Is (2005)
- Just like You (2007)
- A Different Me (2008)
- Keyshia (2010)
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Televisheni
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina |
---|---|
2005 | All of Us (Mgeni Mwalikwa) |
2006–2008 | Keyshia Cole: The Way It Is |
2008–2010 | Snoop Dogg's Father Hood (Mgeni Mwalikwa) |
Paris Hilton's My New BFF (Mgeni Mwalikwa) | |
BET's 106 and Park (Mgeni Mwalikwa) | |
BET Awards |
Filamu
[hariri | hariri chanzo]- How She Move (2008) - Kama jina lake
- ATL 2 (2011) - TBA
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Joyner, Joyner. "Radio Host Knows Who Keyshia Coles father is". Telewatcher. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-31. Iliwekwa mnamo 2009-09-07.
- ↑ 2.0 2.1 Birchmeier, Jason. "Keyshia Cole Biography". Allmusic. Iliwekwa mnamo 2008-11-02.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-20. Iliwekwa mnamo 2010-10-11.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-26. Iliwekwa mnamo 2010-10-11.
- ↑ Keyshia Cole Profile – Biography
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Official website Ilihifadhiwa 13 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Kigezo:IMDb