Just Stand Up!

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Just Stand Up!”
“Just Stand Up!” cover
Single ya Artists Stand Up To Cancer
Imetolewa Agosti 21, 2008 (2008-08-21) (digital)
Septemba 30, 2008 (2008-09-30) (CD single)
Muundo Digital download, CD single
Imerekodiwa 2008
Aina Pop, R&B
Urefu 3:34
Mtunzi Babyface, Ronnie Walton

"Just Stand Up!" ni wimbo ulioimbwa na mjumuisho wa wasanii mbalimbali, wanaoimba miondoko ya pop, R&B, rok, na Katri katika tamasha la kukusanya fedha kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa saratani.Mtayarishaji na mtunzi wa nyimbo wa Marekani L.A Reaid aliandaa ushirikiano huo wa wasanii baada ya kukutana na mwanzilishi wa tamasha la Pingana na Saratanai, na kuandaa tamasha litakalosaidia kuchangisha fedha kwa ajili ya kukuza mfuko huo. Waandaaji hawa waliandaa wimbo huu, kwa kushirikiana na waimbaji wa Kimarekani kama vile Bebyface na single hii ilitoka tarehe 21 Agasti 2008

Waimbaji hawa waliimba wimbo huu moja kwa moja ambayo ilirushwa hewani katika vyombo vya habari mbalimbali kama vile ABC, CBS na NBC tarehe 5 Septemba 2008.[1][2] Single hii ilitolewa tena tarehe 30 septemba 2008, na pia ilitoka na nakala ya tamasha la moja kwa moja. Lakini single hii haikuwa na video yake.

Waimbaji[hariri | hariri chanzo]

Onesho la moja kwa moja[hariri | hariri chanzo]

Onesho la moja kwa moja, lilikuwa katika tamasha la Stand Up 2 Cancer lililofanyika tarehe 5 Septemba 2008, lililooneshwa katika vyombo vya habari mbalimbali. Waimbaji wengi walionekana ambao walirekodi wimbo huu isipokuwa, LeAnn Rimes, Sheryl Crow na Melissa Etheridge, na wapo walioongezeka kama vile Nicole Scherzinger kutoka katika kundi la Pussycat Dolls aliyeimba nafasi ya Sheryl Crow.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Just Stand Up!"
  2. "Just Stand Up!" (Live Video)

Chati[hariri | hariri chanzo]

Wimbo huu uliingia katika chati ya Billboard Hot 100 katika wiki ya 78, ya tarehe 13 septemba. Wiki iliyofuatia ilifanikiwa katika mauzo na kuvuka nafasi takribani 67 na kufika hadi nafasi 11. Wiki iliyofuatia wimbo huu ulianguka na kushuka hadi nafasi na 36. Wimbo huu pia ulishaingia katika chati ya Uingereza na kufanikiwa kushika nafasi 39, na baadae kupanda hadi nafasi 26. Katika chati ya nchini Canada wimbo huu ulifanikiwa kufika hadi nafasi ya 10 katika wiki ya septemba 11.

Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (2008) Ilipata
nafasi
Australian ARIA Singles Chart[3] 39
Austria[4] 73
Canadian Hot 100[5] 10
Italian FIMI Singles Chart 7
Japan Hot 100 85
DSM Hot 25 Chart 1
DSM Hot Pop Chart 1
New Zealand RIANZ Singles Chart[6] 19
Swedish Singles Chart[7] 51
U.S. Billboard Hot 100[8] 11
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs[9] 57
U.S. Billboard Pop 100[10] 18
UK Singles Chart 26

Wafanyakazi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kaufman, Gil. "Mariah Carey, Beyonce, Fergie, Miley Cyrus, More Collaborate On Cancer Benefit Single", MTV News, 2008-08-19. Retrieved on 2008-08-20. 
  2. Jessen, Monique. "Mariah Carey, Beyoncé Unite For Charity Record", People, 2008-08-20. Retrieved on 2008-08-26. Archived from the original on 2016-05-05. 
  3. Just Stand Up! chart history - australian-charts.com. australian-charts.com. Retrieved on 28 Juni 2009.
  4. http://www.lescharts.com/showitem.asp?interpret=Stand+Up+To+Cancer&titel=Just+Stand+Up&cat=s
  5. Canadian Hot 100
  6. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-02-15. Iliwekwa mnamo 2010-01-28.
  7. Swedish Singles chart
  8. Billboard Hot 100
  9. Hot R&B/Hip-Hop Singles Sales. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-12-05. Iliwekwa mnamo 2008-12-05.
  10. Billboard Pop 100. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-12-05. Iliwekwa mnamo 2008-12-05.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]