Khanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kanga (kitambaa))
Khanga dukani.

Khanga (au kanga) ni vazi au nguo nyepesi pia ndefu ya rangi ambayo hupendwa kuvaliwa na wanawake, hasa nchi za Afrika Mashariki na Afrika Magharibi. Kanga inafanana na kikoi ambacho kawaida huvaliwa na wanaume.

Kwa kawaida kanga huwa na upana wa sentimita 150 na urefu wa sentimita 110. Kanga huweza kutumiwa kama vazi rasmi, kitambaa cha kichwani, taulo, kitambaa cha mezani na kwa shughuli mbalimbali kama kubeba watoto au kubeba mizigo kichwani.

Hutumiwa pia kama zawadi kwenye sherehe za kuzaliwa, harusi, n.k.[1] Hutolewa pia kwa familia iliyofiwa na ndugu yao nchini Tanzania.

Mwanzoni kanga ilikuwa ikirembwa kwa vitone vidogo ambavyo vilionekana na manyonya ya ndege aina ya kanga. Ndiyo sababu ilipewa jina hili.

Kanga huwa na sehemu tatu: pindo, mji (sehemu ya kati), na ujumbe. Ujumbe mara nyingi huwa ni kitendawili au fumbo.

Hii ni mifano ya ujumbe wa kwenye kangaː

  • Majivuno hayafaif[2]
  • Mkipendana mambo huwa sawa
  • Japo sipati tamaa sikati [2]
  • Wazazi ni dhahabu kuwatunza ni thawabu: [2]
  • Sisi sote abiria dereva ni Mungu[2]
  • Fimbo la mnyonge halina nguvu[3]
  • Mwanamke mazingira tunataka, usawa, amani, maendeleo[2]
  • Naogopa simba na meno yake siogopi mtu kwa maneno yake[2].
  • Leo ni siku ya shangwe na vigelegele

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. John., Picton, (1995). The art of African textiles : technology, tradition, and lurex. Becker, Rayda., Barbican Art Gallery. London: Barbican Art Gallery. ISBN 0853316821. OCLC 34052769. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Alphabetical List of Inscriptions and Their Translations: Kanga & Kitenge: Cloth and Culture in East Africa. Erie Art Museum. Jalada kutoka ya awali juu ya 11 August 2012. Iliwekwa mnamo 18 December 2009.
  3. Howden, Daniel. "Kangalicious: Let your dress do the talking", The Independent, 14 November 2009. Retrieved on 14 November 2009. "Anyone wearing a kanga with the proverb Fimbo La Mnyonge Halina Nguvu" (Might is Right) may know something about the darker side of the garment's journey from the coast into the interior." 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Khanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.