Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma

Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma iko eneo la kaskazini magharibi mwa Kaunti ya Turkana nchini Kenya.[1] Kambi hii ina zaidi ya wakimbizi 200,000. Ni mojawapo ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani. Familia na watoto kutoka Sudan Kusini, Somalia, Ethiopia, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Uganda, na Rwanda wanaishi huko.[2]

Watoto huko Kakuma

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma ilijengwa katika mwaka wa 1992 kwa “Wavulana Waliopotea wa Sudan” au “The Lost Boys of Sudan”.[1] Zaidi ya watoto elfu thelathini walikimbia vita katika nyumba zao nchini Sudan. Watoto hawa walitembea kwa zaidi ya maili elfu moja kwa miezi mitatu. Wavulana wengi na wasichana wachache walikufa kwa sababu ya kuzama, njaa, na mashambulizi kutoka kwa askari. Safari ilikuwa ya mwaka mmoja na nusu, na watoto walikuwa pekee yao. Baada ya mwaka moja, wao walifika katika mji wa Kakuma na UNHCR iliwapa chakula. Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma alianza na “Wavulana Waliopotea wa Sudan” na sasa, wakimbizi wengi kutoka nchi nyingi za Kiafrika huja mpaka Kakuma.[1][3]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Wanafunzi shuleni huko Kakuma

Kambi hii ina watoto zaidi katika shule kulikwa maeneo mengine ya Kakuma. Katika mwaka 2014, 25% ya watoto katika kambi hii walisoma katika shule ya chekechea na kulikuwa na shule saba za chekechea. Pia, 65% ya watoto walisoma katika shule ya msingi na kulikuwa na shule ishirini na moja za msingi. Mwisho, 2% ya watoto walisoma katika shule ya sekondari na kulikuwa na shule nne tu za sekondari katika Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma. Kwa sababu ya tamaduni za watu wengi dhidhi ya elimu kwa wasichana katika Kakuma, kuna vikwazo kwa wasichana kwenda shuleni. Kuna wanafunzi wengi katika kambi hii, lakini 20% tu ya wanafunzi ni wasichana. Hata hivyo, kuna shule za bweni karibu ya Kakuma ambazo ni za wasichana pekee ambazo zinaweza kutumiwa na washichana hawa karibu na Kakuma.[1][3][4]

Nyumba, Chakula, na Afya[hariri | hariri chanzo]

Wakimbizi katika kambi hujenga nyumba zao. Wanapewa baadhi ya vifaa vya kujenga nyumba, lakini wakati mwingi, wakimbizi huhitaji nyenzo zaidi ili kujenga nyumba nzuri, kwa hivyo hali ya nyumba sio nzuri sana. Watu wanatumia mbao, matope, na miwa kujenga nyumba zao.[4] Kuna mikoa minne kambini, na wakati mwingi, watu kutoka nchi moja hujenga nyumba katika eneo moja. Kila jumuiya ina masoko madogo na makanisa. Watu wengi wanahitaji mgao wa chakula kutoka kwa serikali na mashirika katika kambi ili kula. Pia, kambi ina hospitali moja na zahanati ndogo kwa wakimbizi.[1]

Kazi, Pesa, na Umaskini[hariri | hariri chanzo]

Watu wengine wana biashara ndogo katika kambi, lakini watu wengi hawawezi kupata kazi kwa sababu hakuna kazi nyingi katika kambi hii. Mashirika katika kambi inaajiri baadhi ya wakimbizi lakini haiwalipi pesa nyingi. Kwa sababu hii, ni vigumu sana kwa wakimbizi katika kambi kupata pesa. Hili tatizo kubwa katika kambi.[5]

Mashirika[hariri | hariri chanzo]

UNHCR

Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma inadhibitiwa na UNHCR (United Nations High Commissioner for Refugees) ambalo ni shirika linalowasaidia wakimbizi duniani zote. Pia, kambi imedhibitiwa na DRA (Department of Refugee Affairs) baada ya mwaka 2006.[2] Mashirika haya yanadhibiti kambi na yanatoa huduma kwa wakimbizi, kama huduma za afya, chakula, maji, na huduma zingine. Mashiriki mengine, UNICEF, hutoa huduma kwa wakimbizi kama huduma ya afya, eneo za watoto kujifunza na kucheza, huduma za ushauri, mafunzo ya elimu kwa walimu, na ulinzi dhidi ya vurugu. Kuna mashiriki mengine katika Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma ambayo hufanya kazi na wakimbizi na serikali ya Kenya kusaidia watu.[2]

Watu Muhimu[hariri | hariri chanzo]

Kuna wakimbizi kutoka Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma ambao wakawa wanariadha muhimu na wanamitindo.

  • Hali Aden alizaliwa katika Kakuma katika mwaka 1997. Sasa, yeye ni mwanamitindo ambao alipata umaarufu kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuvaa hijabu katika shindano la Miss Minnesota Marekani.[1]
  • Rose Nathike Likonyen aliishi katika Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma pia, na sasa, yeye ni mwanariadha wa uwanjani kutoka Sudan Kusini. Yeye aliwakilisha Timu ya Olimpiki ya Wakimbizi katika mwaka 2016 mjini Rio.[1]
  • Awer Bul Mabil alikuwa wakimbizi ya Sudan Kusini na sasa yeye ni mwanariadha muhimu. Yeye alicheza mpira wa miguu kwa timu ya Australia.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 Manaswi Topale (2022-09-27). "Refugee Camp Kakuma: 10 Facts You Should Know". RTF | Rethinking The Future (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-04-22. 
  2. 2.0 2.1 2.2 "KAKUMA REFUGEE CAMP". UNICEF USA (kwa en-GB). Iliwekwa mnamo 2023-04-22. 
  3. 3.0 3.1 "Kakuma Refugee Camp". Kakuma Girls (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-04-22. 
  4. 4.0 4.1 Broz. "Kakuma Refugee Camp". Seeds of South Sudan (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2023-04-22. 
  5. "Kakuma", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2023-02-27, iliwekwa mnamo 2023-04-22