Kamala Harris

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Kamala Harris
Amezaliwa20 Oktoba 1964
Kazi yakewakili nchini Marekani


Kamala Devi Harris (alizaliwa 20 Oktoba 1964) ni wakili nchini Marekani na mwanasiasa ambaye ni Seneta anayewakilisha jimbo la Kalifornia toka mwaka 2017. Kamala ni mwanachama wa Chama cha Kidemokrasia cha Marekani na alikuwa Mwanasheria Mkuu wa 32 wa Kalifornia kati ya mwaka 2011 hadi 2017 na Mwanasheria Mkuu wa 27 wa San Francisco toka 2004 hadi 2011.

Harris ni mtoto wa profesa Donald J. Harris (*1938), mwenye asili ya Jamaika, na mtafiti wa kansa Shyamala Gopalan (1938-2009), mwenye asili ya Tamil Nadu, Uhindi. Baada ya kutengana kwa wazazi alihama pamoja na mama yake kwenda Kanada hadi mwisho wa elimu ya sekondari.

Nchini Marekani alisoma siasa, uchumi na sheria hadi kuhitimu Uzamivu wa sheria mnamo 1989. Alianza kazi kwenye ofisi za wanasheria wa serikali hadi kuchaguliwa kuwa mwanasheria mkuu wa jiji la San Francisco mnamo 2004 kama mgombea wa chama cha Kidemokrasia, halafu mwanasheria mkuu wa Kalifornia mnamo 2011[1].

Mwaka 2015 alianza kugombea nafasi ya senati ya Marekani akachaguliwa 2016. Mwaka 2019 alitangaza kuanza kampeni ya kuwa mgombea wa Chama cha Kidemokrasia kwa Urais wa Marekani kwenye uchaguzi wa 2020. Alicha kampeni hiyo lakini kwenye Agosti 2020 aliteuliwa na Joe Biden, mgombea wa urais wa Chama cha Kidemokrasia, kuwa mgombea mwenza kama makamu wa rais.

Kitabu[hariri | hariri chanzo]

  • The Truths We Hold: An American Journey Penguin Press, 2019.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kamala Harris kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.